MRADI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI TUMATI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ni kati ya Halmashauri ambayo imenufaika na Mradi wa Program For Results (P4R); Kati ya Miradi iliyofadhiliwa na Program hiyo ni Mradi wa ujenzi wa Shule ya TUMATI ambapo mradi umejenga Maktaba ya Kisasa, vyoo sita, Madarasa manne na Bweni la wanafunzi.
Mradi huo wa ujenzi wa Shule umegharimu fedha za kitanzania shilingi Milioni 141 ambapo mpaka sasa mradi umekaribia kukamilika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara ilifanya ukaguzi wa mradi huo mnamo tarehe 29 Desemba, 2017 ukaguzi huo uliongozwa na Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa, Mhandisi wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa , Katibu wa Afya wa Mkoa na Afisa TEHAMA wa Mkoa.
Ukaguzi huo ulikagua majengo yote na kuonekana kuwa kuna mapungufu na ilishauriwa mapungufu hayo yarekebishwe kabla ya ukaguzi wa mwisho na mradi usipokelewe iwapo marekebisho hayo hayatafanyika ili kuhakikisha thamani ya fedha ambayo mradi umetoa na Serikali inaonekana na inawanufaisha wananchi na wanafunzi wa TUMATI.
UKAGUZI WA MRADI WA UJENZI WA VITUO VYA AFYA VYA TLAWI NA DAUDI HALMASHAURI YA MJI WA MBULU
Mkoa wa Manyara ni moja kati ya Mikoa ambayo imepatiwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya katika Halmashauri zake za Mbulu Mji, Mbulu Wilaya, Hanang' na Simanjiro; Vituo hivi vinajengwa kwa hela ya Serikali kupitia utaratibu wa "false accounts" ambapo Halmashauri zinatumia wakandarasi wadogo (local engineers) katika ujenzi wa Vituo hivyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliunda timu ya ukaguzi wa baadhi ya vituo hivyo katika halmashauri ya mji wa Mbulu vituo vilivyokaguliwa ni pamoja na Kituo cha Afya cha Daudi na Tlawi; Ukaguzi huo ulifanyika mnamo tarehe 29 Desemba, 2017 ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa pamoja na Mhandisi wa Mkoa.
Miradi ya ujenzi wa vituohivyo umefikia hatua nzuri na wananchi wanaifurahia na kuonekana kuwa sasa suala la afya limepewa kipaumbele kwenye Halmashauri zao; Katika ukaguzi huo timu ya Mkoa ilikutana na kamati ya Ujenzi ya Halmashauri na kutoa mapendekezo mbalimbali ya uboreshaji na kushauri wakandarasi na kamati kuhakikisha ujenzi huo unajengwa na kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kuhudumiwa na vituo hivyo.
Mradi ulihusisha ujenzi wa Wodi ya Uzazi na mtoto (Reproductive and Child Health), Chumba cha upasuaji (Theatre), Maabara ya kisasa, Mochwari na Nyumba ya Daktari.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.