• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Kilimo
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu za Kujiunga na Bangdalalu Sekondari
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Habari
  • Blog

Mkirikiti aipongeza Shule ya Lalakir Kiteto kwa kushika nafasi ya kwanza Manyara.

Imechapishwa Tarehe: November 25th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Mkirikiti ameipongeza shule ya msingi Lalakir iliyopo wilayani Kiteto kwa kushika nafasi ya kwanza Mkoa wa Manyara katika matokeo ya Mitihani ya darasa la saba mwaka 2020.

Mhe. Mkirikiti ametoa pongezi hizo jana alipoongea na walimu na wanafunzi wa shule hiyo alipotembelea shuleni hapo kukagua miradi ya Education Performance for Results (EP4R) na ujenzi wa miundombinu ya vyoo bora na miundombinu ya maji kupitia program ya usafi wa mazingira na usambazaji wa maji vijijini (SRWSS).

“Napenda kuwapongeza walimu,wanafunzi,wazazi na wadau wote was hule hii kwa ushirikiano wenu wa kuhakikisha Watoto wetu wanapata elimu bora, na kwa kweli watoto wa wafugaji wakiwekewa mazingira mazuri ya kusoma wanasoma sana!!” Alisema Mhe.Mkirirkiti.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa pia amewapongeza walimu katika shule hiyo kwa kuonesha upendo miongoni mwao na kwa wanafunzi kitu kinachofanya kuongezeka kwa ufaulu shuleni hapo.

Akisoma risala mbele ya Mkuu wa Mkoa, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikishika nafasi yay a kwanza Kimkoa na Kiwilaya kwa miaka mitano mfululizo na mwaka huu wamefanya mitihani wanafunzi 33 na kati ya hao wanafunzi 32 wamefaulu kwa daraja A na Mwanafunzi 1 tu amepata daraja B na shule imepata wastani wa alama 219.1212 ambayo ni daraja A na hivyo kuifanya kuwa shule ya kwanza katika Mkoa wa Manyara

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa mafanikio hay ani matokeo ya upendo na ushirikiano miongoni mwa walimu,wanafunzi, viongozi wa kamati, jamii na serikali kwa ujumla. Aidha walimu wanafanya kazi kwa bidi,ubunifu na kujituma mno kiasi kwamba wanafundisha usiku na siku za mwisho wa juma” Alisema Mwalimu Mkuu wa shule hiyo.

Mara baada ya taarifa hiyo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mkuu wa Mkoa alifurahishwa san ana jinsi walimu wa shule ya Lalakir wanavyoishi kwa upendo na wanafunzi na jinsi wanavyojitolea na pia alianzisha harambee kwa msafara mzima uliombatana nao kuwachangia wanafunzi na kufanikiwa kuchangisha shilingi laki mbili na elfu arobaini na mbuzi mmoja ili wanafunzi wabadishe chakula kwa siku hiyo Pamoja na kuwapatia wanafunzi wa shule hiyo zawadi ya mpira mmoja wa wavulana na kumtaka Mkurugenzi wa Wilaya ya Kiteto Bwana Tamim Kambona kuwaletea mipira ya pete kwa ajili ya wasichana.

                     Mkuu wa Mkoa wa Manayara Mhe.Joseph Mkirikiti akikabidhi zawadi ya Mpira kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Lalakir iliyopo Wilayani Kiteto.

Shule ya msingi Lalakir ni miongoni mwa shule zilizonufaika na  ujenzi wa miundombinu ya vyoo bora na miundombinu ya maji kupitia Programu ya usafi wa mazingira na usambazaji wa maji vijijini (SRWSS) kwa kupatiwa jumla ya shilingi Milioni nane laki nane elfu kumi na saba na mia tano (8,817,500)

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MKOA WA MANYARA December 18, 2020
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA BABATI MJINI October 21, 2020
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018 MKOA WA MANYARA December 27, 2017
  • OR-TAMISEMI YATANGAZA AJIRA MPYA ZA WALIMU WA MSINGI NA SEKONDARI JULAI 2018 July 17, 2018
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Vijana Kiteto wanufaika na Mikopo ya Halmashauri

    January 05, 2021
  • Babati watakiwa kuchangamkia Mikopo ya Serikali

    January 04, 2021
  • Waziri wa Kilimo awataka Wakulima wa ngano kuongeza uzalishaji

    December 24, 2020
  • Njooni muwekeze Manyara- RC Manyara

    December 22, 2020
  • Tazama Zote

Video

Nangwa Sekondari katika muonekano mpya
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 310

    Simu ya mezani: 027-2510066

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: rasmanyara.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2020 Manyara Region . All rights reserved.