• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Babati watakiwa kuchangamkia Mikopo ya Serikali

Imechapishwa Tarehe: January 4th, 2021

Wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Babati wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujipatia mikopo ya asilimia kumi isiyo na riba kutoka Serikalini ili kuweza kujifanyia shughuli zao na kujikwamua na umaskini.

Hayo yamesemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi. Amina Masood wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa wa kuangalia namna gani asilimia kumi zinazotokana na mapato ya ndani kama zinawafikia wananchi kama serikali ilivyoagiza.

"Sisi Halmashauri ya Mji wa Babati tumetenga Milioni themanini kwa ajili ya vikundi vya  wanawake,Vijana na Walemavu lakini mpaka sasa kati ya vikundi kuna vikundi viwili tu vilivyokidhi masharti ya uchukuaji wa mikopo hiyo, hivyo nawasihi wananchi wa babati mjini kuunda vikundi na kuja Halamashauri ili kujipatia mikopo ya serikali kwani mikopo hiyo haina riba” Alisema Bi. Amina Masood.

Akizungumzia mikakati mbalimbali iliyowekwa na Halmashuari ili kuhakikisha wanawake,vijana na walemavu wa Babati  wanaunda vikundi na kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo hiyo Bi. Amina amesema kuwa wao kama Idara ya Maendeleo ya jamii imeweka Afisa Maendeleo ya Jamii kila kata ili wananchi wapate elimu juu ya uundaji wa vikundi na hatimaye waweze kupata mikopo hiyo.

Kwa upande wake Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bw. Khamis Katimba amesema kuwa ili kuhakikisha kiwango cha fedha kinaongezeka kwa ajili ya kutoa asilimia kumi wao wamejipanga kuongeza vyanzo vya mapato katika Halmashauri na kuzuia mianya yote ya wanaokwepa kulipa kodi zinazotozwa na Halmashauri.

“Tutajitahidi kuongeza vyanzo vyetu vya mapato na kuziba mianya yote ya wakwepaji wa kodi za Halmashauri ili kuongeza makusanyo kwani tukiongeza makusanyo hata ile asimia kumi inayotakiwa kwa wanawake,vijana na walemavu itaongezeka”Alisema  Mchumi huyo.

Pamoja na kuwataka wananchi hao kujiunga kwenye vikundi na kwenda Halmashauri kuomba mikopo hiyo vilevile Mchumi huyo alielezea changamoto mbalimbali za zinazojitokeza kwenye mikopo hiyo ikiwemo ya wananchi kudhani kuwa mikopo hiyo ni misaada na hivyo hawapaswi kurejesha na baadhi ya wanavikundi kukimbia ili wasilipe mikopo hiyo.

Akitoa ufafanuzi juu ya dhana ya wananchi kudhani kuwa hawapaswi kurudisha mikopo hiyo Afisa Usimamizi fedha kutoka TAMISEMI  Bwana Ismail Chami alisema kuwa lazima wananchi hao wapewe elimu ili kujua kuwa fedha hizo sio sadaka bali ni mikopo ya kuwafanya wajikwamue kutokana na umasikini ndo maana Serikali inatoa bila riba yoyote.

"Maafisa Maendeleo ya Jamii lazima mkatoe elimu juu ya mikopo hii na wananchi wafahamu kuwa nia ya serikali ni kuwasaidia wananchi wake ndo maana mikopo inatolewa kwa wanawake,vijana na walemavu bila riba yoyote hivyo lazima mikopo hiyo irejeshwe ili wengine waweze kukopa" Alisisitiza Bwana Chami.

Maafisa hao kutoka TAMISEMI pia walipata nafasi ya kwenda kuvitembelea Kikundi cha Mrawa kilichopo Mrara kinachojishughulisha na usindikaji wa nafaka,Viungo vya chai na pilipili, Kikundi cha KIBATIMA kilichopo Mtaa wa Nyunguu kinachojishughulisha na uuzaji wa Mabatiki ili kujionea jinsi walivyotumia mikopo hiyo ya serikali kujianzishia miradi ya maendeleo na kujiingizia kipato na kuwataka Maafisa Biashara wa ngazi ya Halmasahuri kuwatafutia masoko ili wapate kuuza bidhaa zao na waweze kufanya marejesho kwa urahisi.

"Ningependa kuwaambia wana vikundi washirikiane na wataalam wa Halmashauri ili watanue soko na kufikia malengo"Alisema Bwana Fulgence Matemele Mchumi kutoka TAMISEMI.

Serikali imeweka sheria kwa kila Halmashauri kutenga asilimia kumi (asilimia nne kwa wanawake,asilimia nne kwa vijana na asilimia mbili kwa walemavu) kutokana na mapato ya ndani na kuwapa mikopo isiyo na riba ili kuwawezesha kuanzisha miradi na kujikwamua kiuchumi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.