• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Barabara Babati Mji Bomba-Wabunge

Imechapishwa Tarehe: March 14th, 2020

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) jana tarehe 13 Machi, 2020 ilifanya ziara katika Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani  Manyara kwa kutembelea miradi ya Ujenzi wa Barabara za lami na Standi Mpya ya Mabasi ya Babati.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bw. Fortunatus Fwema ( wa kwanza kulia) akiiongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) kukagua barabara za lami mjini Babati.

Wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mh. Vedasto Ngombale Mwiru aliisifia Halmashauri ya Mji wa Babati kwa ujenzi mzuri wa barabara za lami katika mitaa ya Babati kwani Barabara na taa zilizojengwa zinapendezesha mji na kuonekana na mandhari ya kuvutia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mitaro ya kupitisha maji na upandaji wa miti pembezoni mwa barabara.

                                                                                    Sehemu ya barabara ya lami iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Babati.

 “Kwa kweli tumefurahishwa na ujenzi wa Barabara za lami katika Mji wa Babati na tungependa Halmashauri zingine kuja kujifunza kwa hapa” Aliongeza Mwenyekiti wa Kamati.

Pia walizitaka Halmashauri nyingine nchini zenye miradi kama hiyo kuja kujifunza katika Halmashauri ya Mji wa Babati.

Pamoja na kupongeza ujenzi wa Barabara hizo Wabunge hao  walishauri wakati wa ujenzi kuongeza upana wa mitaro ili kujihadhari na mafuriko na pia kuweka sharia ndogondogo zitakazoweza kuzilinda barabara hizo kudumu kwa muda mrefu.

Baada ya kumaliza ukaguzi wa barabara za lami wajumbe wa kamati hiyo pia walitembelea Stand mpya ya Mabasi iliyopo katika eneo la Maisaka katani na kujionea maendeleo katika Stand hiyo.

Akitoa maelezo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bw. Fortunatus Fwema alisema katika eneo hilo kutakuwa na stand ya mabasi, magari ya mizigo, magari madogo,eneo na magari ya kusubiria abiria pamoja na sehemu za huduma za kifedha ili kuwarahisishia wasafiri na watumiaji wa eneo hilo huduma za uhakika.

                                                  Sehemu ya stand Mpya ya Mabasi iliyotembelewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC)

Akitoa malalamiko yake mbele ya Kamati hiyo Mfanyabiashara katika eneo hilo la stand alisema kuwa tatizo ni kuwa Halmashauri imewapa maeneo yenye vipimo vidogo na hivyo kushindwa kupanua  biashara zao na pia kuna changamoto ya eneo la kupunzikia hasa wakati wa mvua kwani eneo lililopo ni dogo mno.

Akiongea wakati wa majumuisho ya ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Vedasto Kingunge alitoa maelekezo kwa Halmashauri kuahakikisha inaongeza ukubwa wa eneo la vibanda na kujenga sehemu nyingi za kupunzikia wasafiri na wafanyabiashara katika eneo hilo.

“Halmashauri hakikisheni mnaongeza ukubwa wa eneo la vibanda vya biashara na kujenga sehemu za kupunzikia ili wanufaika na stand wakae mahali salama na vilevile fanyeni haraka kumalizia stand hii itasaidia kuongeza mapato ya Halmshauri yenu na kuliongezea thamani eneo mlilopima viwanja” Alisongeza Mwenyekiti huyo.


Halmashauri iliamua kuhamishia Stand katika eneo hilo kutoka Mjini ilipokuwa stand ya zamani mara baada ya Chama Cha Mapinduzi kuchukua eneo lao.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.