• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

CHANELI YA UTALII KUVUTIA WATALII WENGI TANZANIA

Imechapishwa Tarehe: January 2nd, 2019

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kuwa chaneli mpya ya utalii inatarajiwa kuvutia watalii wengi zaidi kuja nchini sambamba na kuongeza pato la taifa.

Akizungumza tarehe 15 Disemba  jijini Dar es salaam, alipokuwa akizindua chaneli hiyo ya utalii inayojulikana kama “Tanzania Safari channel” Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kuwa chaneli hiyo mpya itatoa fursa ya kutangaza wanyama mbalimbali waliopo katika hifadhi za wanyama, utamaduni wa watanzania pamoja na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kuvutia watu wengi zaidi kuja kufanya utalii na hatimaye kuongeza kiasi cha fedha kitachochangia katika pato la taifa.

“Chaneli hii ni njia muhimu ya kutangaza utalii ndani na nje ya nchi yetu, ambapo itaongeza idadi ya watu watakaotembelea Tanzania” alisema Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri Mkuu Majaliwa aliongeza kuwa kwa sasa watalii wanaokuja nchini kwa mwaka ni milioni 1.3 , na matarajio ya Serikali ni kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia milioni 2 ifikapo mwaka 2020, hivyo chaneli hiyo ya utalii itasaidia katika kufikia lengo hilo la Serikali.

Naye, Waziri Utalii na Maliasili Dkt. Khamis Kigwangala alisema kuwa sekta ya utalii nchini inachangia asilimia 17.7 katika pato la taifa, na katika mwaka 2017 shilingi trilioni 5.04 zilipatikana kupitia sekta hiyo, na hivyo Serikali imeanza kutekeleza mikakati mbalimbali itakayo saidia kukuza utalii na kuongeza pato la taifa

Akitolea mfano  mikakati hiyo kuwa ni “kuimarisha masoko ambapo wataalamu wa utalii wameshafanya maonesho ya barabarani katika baadhi ya nchi na hivi karibuni watafanya maonesho hayo nchini China ili  kuongeza masoko mapya” alisema Waziri Kigwangala

Waziri huyo wa Maliasili na Utalii, alifafanua mikakati mingine ya wizara hiyo ni kuweka mabango yenye picha mbalimbali za vivutio vya utalii  katika barabara inayoelekea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Aidha, Waziri huyo ametoa fursa kwa wasanii mbalimbali wakiwemo wa filamu na  muziki kutumia sehemu za vivutio vya utalii nchini kwa ajili ya kutengeneza kazi zao za sanaa.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, kutoka Zanzibar,  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Dkt. Saleh Yusuph Mnemo alisema kuwa chaneli hiyo inatarajiwa kuwasaidia watu wengi kufahamu vivutio vya utali vilivyopo nchini sambamba na kuongeza mapato, ambapo Zanzibar peke yake ina vivutio vya mambo ya kale 39.

Naibu Katibu Mkuu huyo, alifafanua kuwa asilimia 80 ya fedha za kigeni zinazopatikana Zanzibar zinatokana na sekta hiyo, huku ikichangia  asilimia 20 katika pato lake la taifa.

 Chaneli hiyo ya utalii inayojulikana kama Tanzania Safari Channel inaonekana kupitia kisimbuzi cha Startimes namba 331, na kurusha matangazo yake kwa lugha mbalimbali

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.