• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account

Imechapishwa Tarehe: February 7th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameonyesha matumizi bora ya utekelezaji wa miradi bila kutumia mkandarasi maarufu kama ‘Force Account ‘ kwa Makatibu Tawala wa Mikoa ,Wenye viti wa Halmashauri, Wakurungezi na Maafisa mipango wa Halmashauri  kwa kuwapeleka kwenye mradi wa Ofisi za Jengo la Ofisi ya Rais TAMISEMI linaloendelea kujengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

Jafo amefanya ziara hiyo baada ya kikao chake cha maelekezo kwa viongozi hao ambao halmashauri zao zilifaulu vigezo na kusaini fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati awamu ya Pili.

Akizungumzia Force Account Jafo alisema kuwa nimeamua kutekeleza kwa vitendo yale ninayowaagiza wakati wote wa maelekezo yangu kuhusu kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yenu.

Katika ujenzi wa Jengo hili la Ofisi za Wizara tuliamua na kukubaliana kwa pamoja kutumia mfumo ule ule ambao unatumika katika halmashauri zetu sio sisi tunatoa tu maagizo lakini hatutendi na sasa kupitia mradi huu tumeamua kuwa mfano halisi wa yale tunayoyazungumza alisema Jafo.

Aliongeza kuwa katika mfumo huu wa force Account tumeweza kusimamia jengo hili kupitia  kamati nne ambazo ni Kamati ya manunuzi, Kamati ya Vifaa, Kamati ya ujenzi na ile ya usimamizi na ufuatiliaji.

“Mradi huu umekuwa na tija pia kwa jamii kwani umetengeneza ajira kwa vijana wetu kwani wao ndo wamekua nguvu katika kufanya shughuli zote za ujenzi kuendelea kwa mujibu wa  maelekezo ya wahandisi ambao wanatokea Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja  na msimamizi wa mradi huu”Amesema Jafo

Wakati huo huo Jafo aliongeza kuwa ujenzi wa Jengo hili la kisasa zaidi linagharimu shilingi billion moja tu Fedha zilizo tolewa na Rais Magufuli kwa kila Wizara kwa ajili ya kujenga Ofisi katika Mji wa Serikali Ihumwa.


“Nataka niwahakikishie kuwa ujenzi wa jengo hilo umeratibiwa na mimi mwenyewe Waziri wa  TAMISEMI ambapo niliwaunganisha  viongozi wote wakuu wa Wizara  pamoja na watendaji wa Wizara ili kuleta matokeo makubwa na ya haraka”

Sasa kama mimi nimeweza wewe kwanini ushindwe na jengo hili limeanza kujengwa mwezi Disemba 2018 na kama mnavyoona sasa hivi jengo limeshafikia hatua ya mtamba wa panya kwahiyo kasi ya ujenzi iko vizuri sana na tutamaliza ujenzi huu ndani ya muda mfupi ujao; Nataka na nyie mkafanye hivi kwenye maeneo yenu alimalizia Jafo.

Kwa kuongezea Jafo amazitaka halmashauri zilizo pata fedha ya kutekeleza miradi ya Kimkakati kuanza mipango ya utekelezaji wa miradi hiyo mapema iwezekanavyo  ili fedha hizo zitakapowasili katika halmashauri hizo miradi ianze mara moja na ili iweze kumalizika kwa wakati uliopangwa.

Aidha  Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Eng. Zenah Saidi ametoa shukrani za dhati kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa fedha hizo na kuhaidi kusimamia kwa umakini na kuhakikisha zinatekeleza miradi husika kwa ufasaha na ubora wa miradi hiyo kuendana na thamani ya fedha hiyo.

“Nitoe wito kwa viongozi wa halmashauri kuwa sasa ni wakati wa kutekeleza miradi hii kwa kutumia mfumo wa Force Account kwani kila mmoja wetu kapata kushuhudia kwa macho yake namna ya mfumo huu unavyo tumika na faida zake kazieleza Bi.Zenah

Kwa kuhitimisha Bi.Zena amewataka viongozi wenzake kuwa makini wakati wa kutafuta wakandarasi wa kutekeleza miradi kwa wengi wao katika makaratasi wanakuwa vizuri lakini katika utekelezaji hakuna kitu.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.