• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

karibu Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Manyara tarehe 13-14 Oktoba 2023

Imechapishwa Tarehe: August 24th, 2023
Na. Phabian Isaya 


Tarehe 14 mwezi Oktoba  ni siku ya kumbukumbu ya  miaka 24 tangu Baba wa Taifa alipoaga dunia. Lakini  tarehe  hii kwa mwaka 2023 nisiku ambayo Mkoa wa Manyara  unapokea  heshima kubwa  ya kuadhimisha siku ya kumbukizi  ya Baba wa Taifa  Hayati Mwalimu Julius  Kambarage Nyerere. Na heshima ya  Mkoa  kufanya  shughuli ya kilele cha mbio za Mwenge kwa mwaka 2023  ni heshima kubwa  iliyopewa Mkoa wa Manyara.

Sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru Mkoani Manyara  ni neema katika mambo mengi  kwanza ni kupokea ugeni wa Mwenge wa uhuru. Ambao ni alama ya amani na umoja katika Taifa letu  Mwenge  wa huru utawasili Mkoa wa Manyara katika Wilaya ya kiteto tarehe 7 mwezi Oktoba  niwazi kuwa  Mwenge utapita  katika  wilaya  za Mkoa wa Manyara na  utafanya  uzinduzi wa miradi mingi.

Katika makala hii tuna angalia jinsi ambavyo Mwenge wa uhuru ujio wake na kilele chake kufanyika Mkoa  wa Manyara utaenda kuleta mabadiliko ambayo yataenda kugusa maisha ya wananchi wa Mkoa wa Manyara. Nakuongeza kasi ya uchumi kwa mtu mmoja mmoja  nihakika kuwa Mkoa wa Manyara utapokea ugeni mkubwa ambao niwa  Rais  wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania   Samia  Suluhu  Hassani.

Miongoni mwa kitu kizuri  ambacho Mwenge wa uhuru utaenda  kuweka alama kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara ni ujenzi wa uwanja wa kisasa wa kwaraa. Uwanja ambao ndipo zitafanyika sherehe za kilele cha mbio za Mwenge  hii itakuwa ni alama kubwa ambayo wananchi wa Manyara na Halmashauri zake hawata weza kusahau kwa miaka mingi katika fikra zao.

Ni uwanja ambao hata mala baada ya sherehe za kilele cha mbio za Mwenge bado utaendelea kuwa kitega uchumi na chanzo cha kuingiza mapato Mkoa wa Manyara. Lakini kutakuwa na mapinduzi makubwa  kwenye Sekta ya michezo katika Mkoa wa Manyara  huwenda Mkoa  ukapata  timu itakayokuwa  ikiwakirisha Mkoa wa Manyara katika ligi kuu ya Tanzania.

Kilele cha Mwenge wa uhuru Mkoa wa Manyara ni fursa kwa vijana wa Mkoa wa Manyara kwanini ni fursa kwa vijana  kuna  namna mbii katika fursa hizo. Mosi  ni fursa ya maonesho ya wiki ya vijana kitaifa ambayo yatafunguliwa  na Waziri Mkuu  Mh. Kasimu  Majaliwa  Majaliwa hii ni fursa kwa vijana wa Manyara  kuonesha  ubunifu wao shughuli zao  kwa namna yake  huu ni mwanzo wa vijana wa Manyara kuonesha vijana wengine kutoka mikoa tofauti  uwezo wao na maarifa yao waliyonayo.

Wiki ya vijana  itawapa wigo mpana vijana wa Mkoa wa Manyara na mikoa mingine inayotarajiwa kushiriki kwenye  wiki hiyo,  kufamiana nakubadilishana ujuzi wakimaarifa n.k. lakini kongamano la vijana ambalo linatarajiwa  kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 150 litasaidia  vijana kusema changamoto zao nakujadili  mambo mengi yenye muktadha  wakumfanya kijana kuwa mzalendo na mwenye mafanikioa ndani ya Taifa lake.

Fursa ya pili ni vijana wa Mkoa wa Manyara kujiinuwa kiuchumi au kuweza kubadirisha  maisha yao kupitia kilele cha mbio za Mwenge  14 mwezi Oktoba  2023.

Niwazi kuwa  huu ni ugeni mkubwa ambao Mkoa unaenda kuupokea  boda boda watanufaika kwa usafirishaji wa watu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine  migahawa itapata ongezeko  la wateja kuliko iliyo kawaida  wa miiki wa Hoteli kubwa  wataongeza wigo wa watu.

Mkoa  utaenda kuwa na mzunguko wa fedha ambao kimsingi unatokana na shughuli za kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru.

 Lakini Mwenge wa uhuru kupitia ujumbe wake wa mwaka 2023.   ‘’TUNZA  MAZINGIRA  OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA  VIUMBE HAI NA UCHUMI WA TAIFA’’  ujumbe huu unatukumbusha  kulinda mazingira ilikuondokana na tatizo  la mabadiliko ya tabia ya nchi  linayoweza kujitokeza.

Mwenge wa Uhuru unatutaka kila mtu awe barozi katika utunzaji wa mazingira ikiwa ni upandaji wa miti pia unatukumbusha  kulinda misitu yetu. Mkoa wa Manyara una vivutio vingi vya utalii na mandhari yenye kuvutia  ni jukumu la kila mwananchi kuendelea kuwa sehemu yakutunza uwoto wetu wa asiri  ambao mungu ameubariki  kupitia mbuga zetu Tarangire  Manyara na  milima  mizuri inayo vutia  katika Mkoa wa wetu.

‘’Karibu Mwenge wa uhuru, karibu Manyara Home of  Tanzanite and  Elephant’’

 

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.