• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

KATIBU TAWALA MANYARA AKAGUA UJENZI WA VITUO VYA AFYA NA MABWENI MBULU

Imechapishwa Tarehe: November 29th, 2018

Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bwana Missaile Musa akiambatana na Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Bwana Anza-amen Ndossa,Katibu wa Afya Mkoa Bwana Thomas Malle na Mjumbe wa Kamati ya Afya Mkoa Dkt. Peter Neema  jana tarehe 28/11/2018 amefanya ziara  ya kukagua ujenzi katika viytuo vya afya na mabweni ya wanafunzi wilayani Mbulu ili kuona maendeleo ya ujenzi huo unavyukwenda katika kuwaletea wananchi na wanafunzi huduma nzuri na za haraka.

Ziara ya Katibu Tawala ilianzia huko Dongobesh kwa kuangalia ujenzi wa Kituo cha Afya Dongobesh na kukuta ujenzi wa majengo ya Maabara,Wodi ya wazazi,jengo la kuhifadhia maiti,nyumba ya mtumishi na njia za kutembelea ukiendelea kwa kasi ndogo na kuiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kuharakisha ujenzi wa kituo hicho ikiwa na pamoja na kurekebisha kasoro ndogondogo zilizopo kwenye milango ili kuhakikisha ifikapo mwishoni mwa mwezi Novemba wananchi wa Dongobesh waanze kupata huduma katika majengo hayo kama alivyoagiza Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa ziarani Mkoani Manyara.

Katika kituo cha afya Tlawi Katibu Tawala alikagua wodi za wagonjwa,njia za kutembelea,nyumba ya mtumishi pamoja na maabara na aliwakuta mafundi wakiendelea na hatua za mwisho za ujenzi na kuwataka wasimamizi wa kituo hicho kuanza kupanda miti na bustani kuanzia kipindi hiki cha mvua ili kituo cha Afya kiwe na mandhari ya kuvutia.

Baada ya kutoka katika kituo cha Afya Tlawi Katibu Tawala wa Mkoa alitembelea katika Shule ya Sekondari Chief Sarwatt ili kuangalia ujenzi wa mabweni mawili (moja la wasichana na  moja la wavulana) na kumtaka Mkuu wa Shule hiyo kuongeza kasi ya kumalizia mabweni hayo ili kuhakikisha ifikapo Januari 2019 wanafunzi wote watakaopangiwa kujiunga na shule hiyo wanapata nafasi ya kusoma katika mazingiara mazuri.

Akiendelea na ziara yake katika kituo cha afya Daudi Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara aliridhishwa na hatua zilizofikiwa katika kituo hicho kwani ina vifaa vya kisasa na na majengo yamekamilika ila alishauri katika  katika changamoto ya maji Mganga Mfawidhi wa kituo hicho ahakikishe Tanki la maji lililopo kituoni hapo litafutiwe namna ya kujengewa ili liwe juu kuwezesha maji kutiririka kwenye mabomba hasahasa Maabara.

Akihitimisha ziara yake katika Shule ya Sekondari Gehandu Katibu Tawala Mkoa alikagua ujenzi wa mabweni mawili na kuitaka kamati ya ujenzimkuharakisha ujenzi huo ili kuhakikisha wanafunzi wanapata sehemu salama ya kulala na kujifunzia.

Katibu Tawala wa Mkoa amekuwa akifanya ziara za mara kwa mara katika wilaya zote ili kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri zote zilipo Mkoani Manyara.

(Kwa picha mbalimbali na Video angalia sehemu ya  Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha na Maktaba ya Video)

Imeandikwa Na: Haji A. Msovu

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.