• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Kikao cha maandalizi ya kuelekea kilele cha mbio za Mwenge Mkoa wa Manyara 2023

Imechapishwa Tarehe: July 21st, 2023

Katibu Mkuu ofisi ya waziri Mkuu  Profesa  Jamal Adam  Katundu na katibu tawala Mkoa wa Manyara Mh Karoline Mthapula.

 Julai 20. 2023 amefanya  kikao cha tathimini ya maandalizi ya kilele cha mbioa za mwenge wa uhuru.  Ambapo  itakuwa siku ya kuzimwa kwa mwenge wa uhuru kitaifa Mkoa wa Manyara umepewa heshima kubwa ya  kuzimiwa kwa Mwenge   Mkoa wa Manyara.

Lengo   mahususi katika kikao hicho ikiwa  nikushirikiana  kwa pamoja  ilikufanikisha  maandalizi mazuri  katika kuelekea  siku hiyo muhimu, Aidha  katibu Mkuu ame karibisha ubunifu  katika maandalizi  hayo  ilikuweza  kufanya kilele cha kuzimwa mwenge wa uhuru mwaka 2023  kuwe na utofauti na hasa ikizingatia kuwa Mkoa  wa Manyara umepewa heshima hiyo kubwa kwa mwaka 2023.

Amewashukuru kwa maandalizi  mazuri  katika hatua za awali  kwa kamati nzima ya Mkoa wa Manyara  kwa jinsi wanavyo endelea na ufanisi  wa maandalizi, Sambamba na hivyo  amepokea taarifa ya jumla kutoka  kwenye  kamati  ya Mkoa wa Manyara katika hatua zake  zenye kulidhisha nakutoa muelekeo mzuri.

Mratibu wa mbio za Mwenge  Mkoa wa  Manyara  Samweli Pastory  akiwasilisha taarifa  ya maandalizi  ameeleza kuwa hadi sasa bajeti ya mwenge  iko tayari  ambayo ni Tsh 1,934,317,126, sambamba na hilo mratibu huyo  wa mbio za mwenge Mkoa wa Manyara  ameeleza  kamati ya maandalizi imefanikiwa  kuandaa sare ya Taifa  katika mbio za mwenge  kwa mwaka (2023).

Pia  ameeleza  juu ya maandalizi  ya wiki ya vijana  ambayo yamepangwa  kufanyika  uwanja wa Ccm  Mkoa  wa Manyara. Sambamba na hilo pia kamati  ya Mkoa wa Manyara katika maadalizi yake imefanikiwa kufanya zoezi la upimaji  Afya kwa wanafunzi  wa alaiki, Pamoja na mratibu kuwasilisha taarifa  lakini  kila kamati imewasilisha  taarifa yake mpaka  ilipofikia katika maandalizi.

Kamati ya chakula  Afya  na vinywaji

Kamati hiyo  imefanikiwa  kuandaa watu  wakutoa msaada wa dharuala katika upande wa afya wakishirikiana na madaktari wa Mkoa wa Manyara.

Ikiwa nikatika  namna tatu tofauti namna ya kwanza ni madaktari kwajili ya watu wote  ambapo kutakuwa na shirika la msalaba mwekundu kwajili ya huduma ya kwanza.

Lakini pia kamati imeendaa madaktari  mahususi kwajili ya wageni maalumu  ambao watakuwa wamealikwa, Madaktari kwajili ya kuhudumia vijana  wa alaiki ilikuepusha suala la vijana hao  kuanguka  wakati wa shughuliza  uwanjani zinapokuwa zikiendelea.

Kamati  pia imeandaa usafi wa mazingira kwajili ya uwanja wa kwaraa ili kukinga na kulinda Afya za watu ambao wata hudhuria  katika siku hiyo,

Aidha kamati hiyo itaanda chakula  ambacho  kitakuwa  kwa makundi mablimbali na tayari maeneo  yamekwisha  tengwa na Mkoa kamati  hiyo imewasilisha taarifa hiyo mbele ya jopo zima  ambalo limeambatana na katibu Mkuu kutoka  ofisi ya waziri Mkuu.

Kamati ya ratiba risala na miradi

Kamati imefanikiwa  kuandaa vitambulisho  kwa makundi mbalimbali  ambayo yata hudhuria  katika kilele hicho cha mbio za mwenge, pia imefanikiwa  kufanya uwandaaji wa salamu kwa Mkuu wa Mkoa.

Kamati ya halaiki na hamasa

Kamati hii imefanikiwa  kuandaa vijana wapatao 1200 wa Mkoa wa Manyara  katika ushiriki wa shughuli mbalimbali  hasa katika wiki ya vijana, imefanikiwa kuandaa mpango wa kuhamasisha  upimaji wa  Afya kwa  wananchi wa Mkoa wa Manyara  katika kuelekea kilele cha kuzima mwenge wa uhuru.

 

Kamati ya maonyesho ya wiki ya vijana

Maonyesho ya wiki ya vijana kamati imeandaa kwanzia tarehe 8 – 9 oktoba  maonyesho ya wiki ya  vijana,  kamati imefanya utambuzi wa makundi ya vijana watakao andamana  ikiwa matarajio ya kamati nikuwa na vijana 3000,  Utambuzi wa vijana watakao husika na maonyesho (wajasiriamali).

uwandaaji wa mdahalo utakao husisha  vijana zaidi ya 150 ikiwa nikujadili mambo yanayo wahusu vijana katika  nyanja za kiuchumi na kijamii, ikiwemo mchango wa vijana katika shughuli za kiuchumi na kijamii. Sambamba na hayo pia kamati  imefanya utambuzi wa miradi  ya mkakati  kwajili  ya uzungukaji wa mwenge  lakini  pia uwandaaji wa bonanza la michezo  ya jadi.

Aidha  katibu Mkuu akiambatana na katibu tawala  Mkoa wa Manyara  na jopo la wataalamu kutoka ofisi ya waziri Mkuu, Ametembelea kanisa  la Roho mtakatifu ambalo itafanyika  Misa takatifu  ya kumbukizi ya siku ya kifo cha Mwalimu Nyerere  oktoba 14 ikiwa sehemu ya ukaguzi wa maandalizi  kuelekea siku hiyo ambayo ndio kilele cha mbio za mwenge kitaifa.

Pia  katibu Mkuu (profesa  Jumal Adam katundu) ametembelea  uwanja wa shule  ya Babati day  ambao utakuwa  ukitumika kwajili ya mafunzo kwa   vijana wa alaiki,

Ametembelea eneo la uwanja wa Ccm stendi ya zamani ambao utatumika kwa  maonyesho ya wiki ya vijana  pia amefanya ukaguzi  wa uwanja wa  kwaraa ambao utatumika  kwa shughuli ya kuzima mwenge wa  uhuru, Amefurahishwa na maandalizi  mazuri  yanayoendelea  akizipongeza kamati zote  na uongozi  wa Mkoa  wa Manyara kwa ujumla.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.