• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Limeni kilimo chenye tija ili kuongeza uzalishaji-Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Imechapishwa Tarehe: November 19th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Mkirikiti amewataka wakulima wa mkoa huo kulima kilimo chenye tija na kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ili yaweze kuwanufaisha na kuongeza kipato cha mkulima wa mkoa wa Manyara.

Mhe. Mkirikiti ameyasema hayo leo mjini Babati alipokuwa akifungua kikao kazi cha mafunzo ya uhamasishaji wa matumizi bora ya zana za kilimo kwa wakulima wadogo na wakubwa kutoka wilaya ya Babati na Mbulu

“Tutambue kuwa sekta za kipaumbele za kiuchumi katika Mkoa wa Manyara ni kilimo,ufugaji,madini,utalii na biashara na ndio vyanzo vikuu vya mapato katika Mkoa wetu.Kwa kutambua umuhimu huo ni vyema kwa wakulima wetu kijikita katika kuzalisha vya kutosha ili kujiongezea kipato” Alisema Mhe.Mkirirkiti.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi kutambua kuwa Serkali ya awamuya tano imeweka msisitizo mkubwa kwenye kilimo ili kuongeza tija na kukifanya kilimo kuwa biashara.lengo ni kujihakikishia usalama wa chakula,upatikanaji wa malighafi za viwanda na kupata ziada ya kuuza nje na ili kufanikisha hayo sarikali itahakikisha pembejeo na zana bora za kilimo ikiwemo mbegu,mbolea,viatilifu/dawa na matrekta kwa uhakika na kwa gharama nafuu.

Katika kuhakikisha elimu ya kilimo bora inatolewa kwa wakulima wote wa Mkoa wa Manyara Mhe. Mkuu wa Mkoa aliwataka Wakurugenzi wote katika Halmashauri za Mkoa wa Manyara kuwaelekeza Maafisa ugani wawe karibu na wakulima na kutoa ushauri wa kitaalam wakati wa kilimo ili wakulima waweze kuongeza uzalishaji.

Akiongea wakati wa kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Manyara Bwana Venance Msafiri alisema kuwa madhumuni ya  kikao kazi cha mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakulima wadogo ili waweze kuzalisha kwa tija kwa kutumia zana bora katika uzalishaji.

Kwa upande wa wakulima walionesha kufurahishwa na mafunzo hayo kwani yameweza kuwakutanisha wakulima wadogo na wakubwa Pamoja na kujadili changamoto mbalimbali na kuona namna ya kuzitatua ili mkulima aweze kunufaika na kilimo kwa kutumia zana bora.

“Yaani mafunzo haya yatatusaidia sana kuongeza uzalishaji, na pia nawashauri waandaji wapanue wigo wa kutoa mafunzo mkoa mzima kwani wakulima tukikutana tunaweza kubadilishana uzoefu na kuwa na kilimo chenye tija” Alisama Bi.Stelleh Hombo Mkulima kutoka Mbulu.

Mafunzo hayo ya uhamasishaji wa matumizi bora ya zana za kilimo kwa wakulima wadogo na wakubwa kutoka wilaya ya Mbulu na Babati yameandaliwa na Ofisi ya Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na  Kampuni ya Agri Crop Mechinization na Loan Agro Tanzania

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Miaka Miwili ya Rais Samia Manyara ni Shangwe tupu Miradi ya Maendeleo

    March 18, 2023
  • SERIKALI YATOA MAAGIZO MGOGORO WA ARDHI KIRU

    February 13, 2023
  • MITI MILIONI 10.5 KUPANDWA MANYARA

    January 27, 2023
  • RC MAKONGORO AMESEMA WALIOCHAGULIWA WATAINGIA DARASANI BILA USUMBUFU WOWOTE

    January 23, 2023
  • Tazama Zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru 2022 Mkoa wa Manyara
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.