• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

MAADHIMISHO YA KITAIFA MANYARA

Imechapishwa Tarehe: July 20th, 2022

                        Serikali imepanga kuhesabu kwa mara moja watu wote watakaolala nchini kwenye usiku wa kuamkia siku ya sensa Agosti 23 mwaka huu  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Lameck Nchemba ameyasema hayo mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang' Mkoani Manyara kwenye maadhimisho ya kitaifa ya siku ya idadi ya watu duniani.Waziri Nchemba amemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye ndiye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa Mkoani Manyara. 

Amesema serikali imejipanga na maandalizi yote yamekamilika ili kuhakikisha watu wote nchini watakaolala usiku wa kuamkia siku ya sensa wanahesabiwa kwa mara moja.Amesema mtu ambaye hatashiriki kuhesabiwa kwenye shughuli hiyo itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu atakuwa anarudisha nyuma jitihada za serikali kupata idadi kamili ya watu."Serikali ina mpango wa kuandaa dira ya Taifa ya miaka 25 hivyo sensa ni nyenzo ya maendeleo ya kufahamu idadi ya watu wake hivyo watanzania washiriki kwa pamoja," amesema Dkt Nchemba.Hata hivyo, ametoa rai kwa viongozi wa serikali kuhakikisha sensa ya mwaka huu inakuwa mfano na watu wote kushiriki ili kusaidia Taifa kupanga mipango ya maendeleo.


                 Mwakilishi mkazi wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani na makazi (UNFPA) Mark Bryan Schreiner amesema wakati Dunia inajiandaa kuwa na idadi ya watu bilioni 8 mwezi Novemba mwaka huu, watanzania nao wanapaswa kushiriki sensa itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu. Amesema asilimia 63 ya wananchi wa Tanzania ni vijana wenye umri wa chini ya miaka 25 hivyo watashirikiana na serikali kuwekeza kwa vijana hasa kwenye suala la afya."Pia tutashirikiana na serikali kwenye sensa ya mwaka huu, hivyo jamii ishiriki kikamilifu kuhesabiwa ili kufahamu idadi ya watu, wakiwemo wanawake, wanaume, wazee, vijana, watoto na makundi maalumu," amesema.

          Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Laurence Mfuru amesema maadhimisho hayo yamefanyika Manyara kutokana na mwitikio wa viongozi na jamii ya eneo hilo.
Mfuru amesema mkoa wa Manyara una mwitikio mkubwa wa ufuatiliaji wa idadi ya watu, maendeleo ya sekta ya elimu, afya, maji, kupambana na ukatili wa kijinsia, hivyo ikapitishwa maadhimisho haya kufanyika Manyara.
Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu ya 'Dunia ya watu bilioni 8 kuhimili wakati ujao ni fursa ya haki kwa wote, shiriki sensa kuhesabiwa kwa maendeleo endelevu'. 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.