• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Mafunzo ya matokeo ya Sensa ya mwaka 2022 Mkoa wa Manyara

Imechapishwa Tarehe: July 18th, 2023

Julai  17. 2023  saa  tano asubuhi  jopo la wataalamu kutoka  Ofisi ya Takwimu  ya Taifa  wametoa  mafunzo   kuhusu mrejesho  wa matokeo ya sense  2022.

 Ambapo  mgeni rasimi katika  mafunzo hayo  ni Spika wa Bunge staafu  Kamisaa  wa Sensa  Mh Anna  Makinda. mafunzo  hayo  yenye  kaulimbiu  ya ‘’Mipango jumuishi  kwa maendeleo  endelevu’’

 

Mh  Anna Makinda  ameeleza  utofauti wa  Sensa ya mwaka 2022  na Sensa  silizopita  nikatika  kuhesabu  vitu vyote  ikiwemo majengo kaya   na vitu mbalimbali ikilinganishwa na Sensa  zilizopita  zikijikita katika  idadi  ya watu  pekee, Ameeleza kuwa  Sensa  ya mwaka 2022  imekuwa na uchakataji  wa taarifa mpaka  kwa makundi maalumu.

Amewataka washiriki  katika mafunzo hayo mafupi  kutumia  fursa  ya mafunzo hayo kwajili ya kwenda kuwezasha ufanikishaji  wa uboreshaji  wa  huduma za kijamii.

 Pia  ameeleza  ahadi za viongozi  nilazima  ziendane na Takwimu  halisi  ya watu  lakini pia  Kamisaa  huyo wa Sensa  amewataka  washiriki  katika mafunzo hayo ya muda mfupi  kufikisha  mafunzo hayo hadi  kwenye ngazi za wilaya.

Ameeleza juu ya wajibu wa  Serikali  kubuni vyanzo vya ajira  kutokana na ongezeko la watu hasa  vijana  ambao ndio nguvu kazi ya Taifa, sambamba na hivyo amewataka vijana kutumia  fursa zinazowazunguka  kuweza  kujiajiri wenyewe.

Lengo  la mafunzo  hayo ikiwa  nikuweka  uwiyano hasa katika miradi  inayoanzishwa na Serikali katika Sekta ya Elimu na Afya, Ikiwa pia nikufanya  urahisishaji wa shughuli za Serikali kwa ujumla  ilikuweza kuendana na ongezeko la watu sambamba na kuongezeka kwa  uelewa  wa watu.

Katika  mafunzo hayo katibu Tawala  Mkoa  wa Manyara  Mh Karolina  Mthapula  amewaeleza washiriki  kuwa  Mkoa  wa Manyara  ulipata bahati  ya kufanya majaribio ya Sensa  mwaka 2021 – septemba,   Ambapo  Kamisaa wa Sensa ndiye  aliye fanya shughuli hiyo , Ametoa  shukrani zake za dhati  kwakuweza  kupata  nafasi  hiyo kwa malanyingine tena katika Mkoa wa Manyara.

Mwenyekiti wa  mafunzo hayo Mh Queen Sendiga  (Mkuu wa Mkoa wa Manyara) ametoa  shukrani  kwa ofisi  ya Takwimu ya Taifa, pia  amewataka watumishi  wa Serikali waliyo hudhuria  mafunzo hayo  kuyaweka  katika  mipango yao ya kazi  ilikuweza kufikisha huduma za kijamii kulingana na uhitaji  wa idadi ya watu.

 Kupitia  mafunzo hayo  mafupi  imeonyesha  Mkoa wa Manyara unaidadi ya watu Milioni moja na lakinane na tisini na mbili kwa  Sensa ya mwaka 2022   ikiwa niongezeko kubwa la watu zaidi,  Ambapo Sensa   ya mwaka 2012  Mkoa wa Manyara ulikuwa na idadi ya watu laki tisa. Lakini Mkoa wa Manyara una Almashauri 5 na wilaya yenye watu wengi ni wilaya ya Babati yenye  idadi ya watu 129,572,

Mkoa  wa Manyara  unaongezeko la watu kwa asilimia 32.4  ambapo Halmashauri  ya Babati inaongezeko la watu Asilimia 37.8,  Ambapo wilaya ya kiteto inaongezeko la asilimia  31.6,  ikiwa ndio ongezeko  la  watu kwa asilimia chache kwa  Halmashauri  zote za  Mkoa wa Manyara, Halmashauri ya wilaya ya Mbulu  ina idadi ya asilimia  6.8  ikiongoza kwa idadi  hiyo  kwa  upande  wa wazee kwa Mkoa wa Manyara.

               ‘’mipango  jumuishi kwa maendeleo  endelevu’’ 


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.