Jana Julai 29,2020, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Manyara imetaifisha Madini ya Tanzanite yenye uzito wa gramu 132.64 yenye thamani ya shilingi Milioni 18,446,894.14 yaliyokutwa kwa Mfanyabiashara wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, kinyume na Sheria.
Mfanyabiashara huyo wa madini ya Tanzanite wilayani humo Lucas Liaseki amekamatwa na kufikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara mbele ya hakimu mkazi Simon Kobelo baada ya kujaribu kutorosha madini ya Tanzanite katika geti la ukaguzi wa madini hayo huko Mirerani.
Wakili Mwandamizi wa serikali ambaye pia ni mkuu wa mashtaka mkoa wa Manyara Mutalemwa Kishenyi amesema mfanyabishara huyo alikamatwa kwa kosa la kutokuwa na kibali cha uchimbaji madini ndo maana serikali imeamua kutaifisha madini hayo.
Aidha amesema mahakama imetoa adhabu ya kifungo cha nje cha miezi 12 na kumuamuru asifanye kosa lolote kwa kipindi hicho.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.