Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe.Queen Cuthbert Sendiga leo tarehe 12 Julai,2024 ameongoza umma wa wananchi wa Manyara kuupokea Mwenge kutoka Mkoani Singida.
Akizungumza wakati wa shamrashamra za mapokezi ya Mwenge katika Kijijo cha Gehandu Wailaya ya Hanang', Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa ukiwa Mkoani Manyara Mwenge wa Uhuru utatembelea miradi 57 yenye jumla ya thamani ya Tsh Bilioni 149.5.
RC Sendiga kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Manyara ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhi Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwisho amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maeneo ambapo Mwenge wa Uhuru utapita.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.