• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Mawaziri Nane Watoa suluhu ya Mgogoro wa Mkungunero,Tarangire

Imechapishwa Tarehe: February 19th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Manyara Mh.Alexander Mnyeti  amepokea ugeni wa Mawaziri Nane wa Serikali ya awamu ya tano Wilayani Simanjiro katika kijiji cha kimotorok leo ziara  ambayo inalenga kutatua migogoro kati ya wananchi waishio katika vijiji vya orbokishu na wananchi wa kijiji cha kimotorok dhidi ya wahifadhi wa Pori tengefu la Mkungunero na hifadhi ya Tarangire.

Kamati hiyo imetokana na kamati iliyoundwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa chini ya Mwenyekiti Waziri wa Ardhi Mh. William Lukuvi na kuwateua Mawaziri wa Kisekta ikilenga kupata maoni, kujionea, kujiridhisha na kuandaa taarifa itakayomshauri Rais katika suala zima la kutatua Mgogoro huo kati ya wafugaji na wahifadhi wa wanyamapori katika maeneo hayo.

Akiongea katika ziara hiyo Mh. Lukuvi alinukuu kauli ya Rais aliyosema “Vijiji vyote vilivyo Ndani ya Hifadhi vibaki kama vilivyo”

 Lukuvi alitia mkazo katika hili kwa kuwaeleza wahifadhi wasiwabughudhi wananchi kwani wanamkasirisha Rais. “wamasai hawakati miti wala hawali nyama pori, kwa sasa tumekuja kuwakumbusha tu mtambue nini Rais wetu anataka” alisema Lukuvi.

Wakizungumza mara baada ya mkutano huo wananchi wa Kijiji cha Kimotorok walifurahishwa sana na ujio huo wa Mawaziri katika eneo lao na kuwa na uhakika wa kuishi kwa amani bila bugudha yoyote.

(Kwa picha mbalimbali  angalia sehemu ya  Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)

Imeandikwa na:Haji A.Msovu

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.