• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Mifumo ya ukusanyaji wa taarifa za Ustawi wa Jamii yatakiwa kuungana

Imechapishwa Tarehe: January 28th, 2019

Mkurugenzi Msaidizi  wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi, Rasheed Maftah ameitaka mifumo inayokusanya taarifa za ustawi wa jamii katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuungana na kuwa  mfumo mmoja unaotoa taaarifa zote zinazohitajika katika kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Maftah ameyasema hayo wakati wa kikao maalum cha kuwapitisha wataalamu na wadau kwenye mfumo wa Ustawi wa Jamii wa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi (MVC-MIS) unaowezeshwa na Taasisi ya MEASURE Evaluation; Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa Reform OR-TAMISEMI mwishoni mwa juma lililopita.

Kupitia kikao hicho  wataalamu wa mifumo hiyo  waliweza kuwapitisha wadau kwenye mfumo unaoenda sanjari na MVC-MIS ambao ni USSD unaowezeshwa na Taasisi ya pact kizazi kipya.

Maftah alisema ni wakati sasa waataalamu wetu kukutana pamoja na kuona namna gani mifumo hiyo ambayo inakusanya taarifa za ustawi wa jamii kuungana na kuwa na mfumo mmoja ambao utafanya kazi zote zinafanywa na mifumo hiyo kwa sasa.

Aliongeza kuwa kazi hiyo ni lazima ifanywe na wataalamu wa mifumo toka Ofisi ya Rais –TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya wakishirikiana na wale waliotenegneza mifumo hiyo hapo awali kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Measure Evaluation pamoja na Path Kizazi Kipya.

“Ni wakati sasa wa wataalamu wetu kujengewa uwezo na kuifahamu mifumo hii kwa undani na kushiriki katika kuiunganisha ili hapo baadae miradi itakapomaliza muda wake na kuikabidhi mifumo hiyo kwa Serikali tuwe na wataalamu watakaoweza kuindeleza na kuisimamia wadau wetu wanavyofanya sasa” alisema Maftaha.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Angelista Kihaga akichangia wakati wa kikao hicho alisema hata kama mifumo hii inawezeshwa na wafadhili lazima waangalie uwezekano wa kuwajengea uwezo zaidi watumishi wa Serikali  ambao wataendelea kuihudumia mifumo baada ya mradi kwisha  kuliko kuajiri watumishi wa muda au kuwajengea uwezo wataalamu wa kujitolea “Volunteers” ambao huondoka mara tu mradi unapomaliza muda wake.

“Sisi kama Serikali lazima tuangalie namna ambavyo mifumo hii inakua endelevu na sio siku  wadau  wakitukabidhi mifumo baasi ndio inakua mwisho wa matumizi ya mifumo hiyo sio sawa; Imefika wakati  ambapo  wataalamu wanatakiwa kufahamu kila kitu katika  mifumo hii ili waweze kuiendeleza hapo baadae” alisema Kihaga.

Awali akiwapitisha wataalam katika Mfumo wa MVC-MIS   Bi. Immaculate Ayebazibwe  Kutoka MEASURE Evaluation alisema kuwa mfumo wa MVC-MIS unawezesha ukusanyaji wa takwimu sahihi zinazofanikisha  upatikanaji wa taarifa za utawi wa jamii, na pia unafanya uchambuzi wa kina wa tawkimu hizo.

Naye Mtaalamu kutoka Pact Kizazi Kipya Bw. Tumaini Mbwambo ambao anasimamia  mfumo wa USSD wa kukusanya taarifa za ustawi wa jamii alisema kuwa mfumo wao unakusanya zaidi  taarifa binafsi  tofauti na ule wa MVC-MIS unaokusanya taarifa kwa makundi.

Wakati huo huo mtaalamu kutoka TASAF Bw. Sesil Latemba alipata furasa ya kuwapitisha wajumbe kwenye mfumo unaotumiwa na TASAF katika kukusanya taarifa za Kaya Masikini kuomba kikao hicho kuona uwezekano wa kuunganisha  mfumo huo na ule wa usatwi wa jamii.

Mfumo huu wa kielektroniki wa  ukusanyaji wa taarifa za watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi wa MVC-MIS unatumika katika halmashauri 67 Nchini na hivi karibuni utafikishwa kwenye halmashauri 106.

Mfumo huu umekuja kuhuisha  ile njia ya awali ya kutumia regista Namba 1 ambayo hutumika kuorodhesha majina ya watoto wote wanaoishi kwenye mazingira hatarishi  katika kijiji au mtaa husika ambao kwa kila mdau anayehitaji kusaidia watoto hao inamlazimu kupitia regista hiyo kuona majina ya watoto wanaohitaji msaada wa kiustawi.

Na: TAMISEMI

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.