• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Kilimo
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu za Kujiunga na Bangdalalu Sekondari
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Habari
  • Blog

Mkirikiti azitaka Taasisi za fedha kutoa mikopo kwa Watu wenye makundi maalum.

Imechapishwa Tarehe: September 18th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Mkirikiti amezitaka taasisi mbalimbali za kifedha zilizomo Mkoani humo kutoa  mikopo kwa makundi mbalimbali ya wenye ulemavu ili makundi hayo yapate mikopo na kuweza kujikwamua kutokana umasikini.

Aliyasema hayo jana katika warsha ya wajasiriamali ambao ni walemavu wa kusikia (viziwi)  iliyoandaliwa  na tume ya ushindani (FCC) ambayo ililenga kuwapa  elimu ya kutambua na kuepuka kununua bidhaa bandia zinazozalisha na watu mbalimbali ambao hawana nia njema na jamii.

"Niwaombe taasisi za kifedha ziwazeshe wajasiriamali walevu ili waweze kunufauke kupitia vikundi vyao" Alisema Mhe.Mkirikikiti.

Pamoja na kuzitaka taasisi hizo za  kifedha Mkoani humo Mhe.Joseph Mkirikiti ameeleza kuwa mtu anayetengeneza bidhaa bandia anakusudia kupata faida kubwa na asiyostahili na ndio maana hazingatii vigezo na masharti katika utengenezaji wake na wamekosa  uzalendo kwa nchi pamoja na watu wake hivyo  serikali haikubaliani nao.

Alisema kuwa mtu ambaye anazalisha bidhaa bandia haishii tu kukosa uzalendo bali anadhamira ya kukwepa kodi hali inayopelekea kudhoofisha uwezo wa serikali katika kuwahudumua watu wake na jambo hilo maana yake siyo kuathiri tu watumiaji wa bidhaa hizo kwa sasa bali anaathiri na kizazi kijacho hivyo ni lazima kuunganisha nguvu zetu kukataa huduma za namna hiyo.

“Na nyie kwasababu ni wajasiriamali hamna budi kwa bidhaa zile ambazo mnashiriki kuzitengeneza najua mnaweza kutengeneza sabuni za maji na wengine mnatengeneza bidhaa za mapishi kama mafuta na viungo   ni vizuri mkaepuka matumizi ya bidhaa ambazo hazina ubora na pia jengeni mazoea ya kutumia viungo vyetu vya ndani ambavyo ndio vinaubora zaidi,

 “Zaidi sana niwaombe wazalishaji wa bidhaa zote bandia zinazotumika na wanadamu kuacha kuzitengeneza nchi yetu siyo eneo la kutupa  takataka,watanzania siyo watu wa kutumia bidhaa za hovyohovyo”alisema Mkirikiti.”

Naye Mkurugenzi Mkuu   wa tume ya  ushindani na  uthibiti wa bidhaa bandia Godfrey Mshana alieleza kuwa semina hiyo ni mhimu kwa Mkoa wa Manyara kwani   ni miongoni mwa Mikoa ya pembezoni  ambayo endapo  itakabiliwa na changamoto za bidhaa bandia  watu wengi wataathirika kabla ya changamoto hiyo haijapatiwa uvumbuzi .

Elimu ni silaha bora zaidi  ya kuweza kupambana na bidhaa bandia kuliko hatua za utekelezaji wa sheria ambayo   huchukua muda wa matunda yake  kuonekana.

Alisema kundi la walemavu ni kundi  muhimu kupewa ulinzi wa kipekee dhidi ya athari za bidhaa bandia kwa ni lina mahitaji maalumu hivyo unapolifikia kundi hilo kwenye  masuala ya elimu unakuwa umewafikia wananchi wote.

 “Katika siku zijazo tume ya kuthibiti bidhaa bandia inafikiria namna bora na yenye ufanisi zaidi ya kupeleka elimu kwa makundi maalum ya walemavu  hususani wenye ulemavu wa kusikia na kuona kwa kuwa ndi mafunzo yenye changamoto na uhitaji mkubwa wa elimu ya jinsi ya kuthibiti na kuepuka bidhaa bandia”alisema Mshana.

Neto Mhadisa ambaye ni mshiriki wa mafunzo hayo ambaye pia ni katibu wa chama cha visiwi  Mkoa wa Arusha visiwi wengi wamekuwa wakishindwa kutambua bidhaa feki kutokana na kutokuwa na elimu huku akisisitiza kuwa viziwi wengi hwajui kusoma hivyo inawawia vigumu kutambua kama ni bidhaa feki.

Aliomba pia Mkuu wa Mkoa kuweka mkalimani katika ofisi yake ili watu wenye ulemavu wa kusikia waweze kupata huduma katika ofisi yake kwani tatizo kubwa lipo kwenye mawasilano na wao kama viziwi wanatumia lugha ya alama ambayo watu wengi hawajui kuitumia.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MKOA WA MANYARA December 18, 2020
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA BABATI MJINI October 21, 2020
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018 MKOA WA MANYARA December 27, 2017
  • OR-TAMISEMI YATANGAZA AJIRA MPYA ZA WALIMU WA MSINGI NA SEKONDARI JULAI 2018 July 17, 2018
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • RC Manyara amaliza Mgogoro wa ardhi baina ya mwekezaji na wananchi

    September 01, 2021
  • Mkirikiti amkabidhi Makongoro Ofisi rasmi

    May 25, 2021
  • Karibu Manyara Mhe. Makongoro Nyerere!!!

    May 22, 2021
  • Tuweke uzalendo ktk kusajili watoto chini ya miaka mitano - RC Manyara

    April 20, 2021
  • Tazama Zote

Video

Asilimia mbili ya mikopo kwa walemavu
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 310

    Simu ya mezani: 027-2510066

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: rasmanyara.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2021 Manyara Region . All rights reserved.