• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Mkoa wa Manyara kuendelea kutoa Chanjo kwa mfumo Jumuishi (Integrated Vaccination Approach)

Imechapishwa Tarehe: April 24th, 2023

Nyeneu, P. R - Mjini Babati

Katika kuhakikisha kuwa jamii inaelewa umuhimu wa chanjo hapa nchini, kila  mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha wiki ya Chanjo kila ifikapo wiki ya mwisho ya mwezi Aprili ambapo kitaifa maadhimisho haya yamefanyika leo tarehe 24 Aprili, 2023 Mjini Babati Mkoani Manyara. Wiki ya Chanjo Duniani ni wiki muhimu katika kuhamasisha Wananchi wote Ulimwenguni ili wawe na uelewa na umuhimu wa Chanjo na athari zinazotokana na kukosa Chanjo ambazo ni pamoja na ulemavu wa kudumu na vifo hususani kwa watoto chini ya miaka mitano. Hayo yemesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ambaye amemwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (MB) ambapo kwa mwaka huu maadhimisho yana kauli mbiu isemayo "Tuwakinge wote  Kwa Chanjo” pia ikienda sambamba na ujumbe usemao “Jamii lliyopata Chanjo, Jamii Yenye Afya”.

Mganga Mkuu huyo ameendelea kusema kuwa Wizara ya Afya iliweka huduma ya Chanjo kuwa kipaumbele cha kwanza kati ya vipaumbele vyake kumi  kwa mwaka 2022/2023. Katika kufikia malengo ya kipaumbele hiki, Wizara imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya huduma za afya ili kuhakikisha walengwa wote wanapata Chanjo. Dhumuni la Wizara ni kuendelea kuikinga jamii ya Watanzania dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo ambayo ni Kifua kikuu, Donda Koo, Kifaduro, Polio, Surua, Rubella, Pepo punda, Homa ya ini, Homa ya uti wa mgongo, Kichomi, Kuhara na Saratani ya shingo ya kizazi. Sambamba na Chanjo hizi, Wizara pia inatoa Chanjo za UVIKO-19 kwa watu wote wenye umri kuanzia Miaka 18 na kuendelea.

Aidha, Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Karoline Mthapula pamoja na wananchi wote wa Mkoa huo wameishukuru serikali kwa Mkoa wa Manyara kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa uzinduzi wa wiki ya Chanjo Kitaifa. “Mkoa ulipokea maelekezo kuhusu pendekezo la uzinduzi huu kufanyikia Kitaifa katika Mkoa wetu wa  Manyara na tuliridhia kwa kuamini maadhimisho haya yatakuwa na faida kwetu”  Alisema Katibu Tawala. Pia Bi. Karoline ameendelea kuwashukuru Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), JHPIEGO kupitia miradi ya Afya Yangu na MCGL, Clinton Health Access initiative (CHAI), Save the Children na pia kuwapongeza wananchi wote wa mkoa wa Manyara kwa namna wanavyoitikia na kutumia huduma za afya ikiwemo huduma za chanjo.

Aidha, Katika kuadhimisha Wiki hii ya Chanjo mkoa utaendelea kutoa Chanjo kwa mfumo jumuishi (integrated vaccination approach) ikijumuisha Chanjo zote katika vituo vya huduma kwa walengwa. Zoezi hili litaanza leo tarehe 24 Aprili hadi tarehe 30 Aprili katika Halmashauri zetu zote. Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara wanaitumia vizuri wiki hii kwa kuwapeleka walengwa wote kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kupata chanjo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.