• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Mkoa wa Manyara wawataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Corona

Imechapishwa Tarehe: March 19th, 2020

Mkoa wa Manyara umeanzisha mpango wa dharura wa kuhakikisha wananchi wanajikinga na homa inayosababishwa na virusi vya Corona, kwa kuwapatia uwezo timu ya wataalamu wa afya mkoa na wilaya ili waweze kukabiliana na mlipuko huo endapo utatokea.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Manyara  amesisitiza kuwa mkoa huo umejiandaa vyema kutoa elimu kwa wananchi ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa COVID 19 ambao kwa sasa umeshawakumba watu watatu.

Amezungumza hayo Mganga mkuu wa mkoa wa Manyara Dr.Damas Kayera  kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara jana Machi 18 akitoa taarifa kwa waandishi wa habari namna walivyojipanga kukabiliana na virusi vya Corona.

Amesema wanatumia njia mbalimbali kama vyombo vya habari katika kutoa elimu kwa wananchi na kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya, namna ya kuchukua tahadhari ya kujikinga na  ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo na ukitokea wafanye nini.

Amesema pia tayari mkoa umeshandaa vifaa pamoja na mazingira ya kutolea huduma kwa mwathirika atakaebainika kuwa na ugonjwa huo.

Alipoulizwa kuhusu upatikanaji wa vipimo vya kutambua kama mtu ameambukiwa, amesema njia inayotumika kutambua wagonjwa wa Korona ni kufanyiwa vipimo vya maabara katika Maabara Kuu ya Taifa ya Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam.

Amewaambia wananchi wasiwe na wasi wasi kwa sababu serikali imejipanga vizuri kuweza kuwahudumia ila wazingatie kuchukua tahadhari.

Afisa afya mkoa wa Manyara Evance Simkoko amesema Kirusi cha Corona kinaenea kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kwa njia ya kukohoa,kupiga chafya au maji maji ambayo sio rahisi kuonekana kwa macho.

Ameyataja mambo muhimu ya kuzingatia ili jamii iweze kukabiliana na kirusi hicho ni pamoja na kunawa mikono kwa sabuni kwa  kutumia maji yanayotiririka kila baada ya kumaliza kufanya jambo lolote au kuingia na kutoka popote pamoja na kuepuka kugusana na mtu yeyote.

Hata hivyo mlipuko wa Ugonjwa huo haujaripotiwa kufika katika mkoa wa Manyara.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.