• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Mkuu wa Mkoa afurahishwa na Mradi wa Maji wa Bilioni mbili

Imechapishwa Tarehe: February 9th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joseph Mkirikiti amefurahishwa na mradi wa maji wa Mayoka- Minjingu unaogharimu shilingi bilioni mbili unaojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Februari 2021.

Mhe.Mkirikiti ameonesha furaha hizo jana baada yaye na kamati ya siasa Mkoa wa Manyara kutembelea mradi wa maji Mayoka-Minjingu unaosimamiwa na RUWASA na kuwakuta mafundi wanaojenga mradi huo wapo katika hatua za mwisho za kuunganisha bomba kilomita 13 kukatiza kati kati ya ziwa Manyara ili kukamilisha mradi huo.

Mara baada ya kufika katika chanzo cha ujenzi huo katika Kijiji cha Mayoka Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Siasa walipata maelezo kutoka kwa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara Mhandisi Wolta Kirita ambaye alisema kuwa mradi huo mpaka sasa wameshalaza bomba kilomita 4 kutoka kwenye chanzo hadi Kijijini hapo na Kilomita 10 zimelazwa ziwa Manyara na fedha zinazotumika kukamilisha mradi huo zinatoka RUWASA Makao Makuu na mara baada ya kukamilika unatarajia kuhudumia wakazi zaidi ya 15000 katika vijiji vya Olasiti,Minjingu,Kakoi, Vilima Vitatu na Mayoka.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa mradi huu unasimamiwa na RUWASA wenyewe na mpaka utakapokamilika utatumia shilingi bilioni mbili na tunatarajia utamaliza kero ya upatikanaji wa maji katika kata ya Nkaiti na baadhi ya vijiji vya kata za Mwada na Magara” Aliongeza Mhandisi Wolta Kirita.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara pia alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa mradi huo utamalizika Mwishoni mwa mwezi februari 2021 baada baada ya kushindwa kumalizika Disemba mwaka 2020 kutokana na changamoto ya mvua iliyosababisha ziwa kujaa.


“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Mradi huu ulitazamiwa kumalizika Disemba 2020 lakini kutokana na changamoto za mvua na kwa sasa tumeazima boti kutoka Halmashauri ya Mji Babati na Halmashauri ya Wilaya ya Babati ili kuhakikisha mradi unakamilika Februari 2021 na ili wananchi waanze kupata maji safi na salama” Alisisitiza Mhandisi Kirita.

Akielezea jinsi alivyofarija na jinsi RUWASA wanavyohakikisha mradi huo unakamilika Mheshimiwa Mkuu aliwapongeza RUWASA kwa kukamilisha miradi ya maji katika Mkoa wa Manyara hasa katika mradi huo wa Mayoka-Minjingu.

“Mimi na kamati ya siasa Mkoa tumefarijika sana kuona mradi huu umefikia asilimia 80 na Meneja wa RUWASA kutuhakikishia kumalizika ifikapo Februari 2021 na pia tumeona kabla mradi kwisha wananchi wa Kijiji cha Mayoka wanaendelea kupata huduma kupitia bomba kuu kabla kuunganishiwa katika vituo vya kuchotea maji” Alisema Mhe.Mkirikiti. 

Wakielezea furaha yao wananchi wa Mayoka wamesema kuwa wameridhika na mradi huo kwani katika Kijiji chao watawekewa vituo 8 vya kuchotea maji na hivyo kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata maji.

“Kiukweli sisi wana Kijiji tumefurahi sana kuletewa maji na Serikali yetu kwani zamani tulikuwa tunakunywa maji kutoka ziwani ambayo siyo salama lakini kwa sasa tumeshaanza kunywa maji safi na salama na baada ya RUWASA kutujengea hivyo vituo vya kuchotea maji na sehemu za kunyweshea mifugo yetu hali itakuwa nzuri sana!! Na tunaahidi kuutunza mradi huu ili usiharibiwe” Alisema Mama Isabela wa Kijiji cha Mayoka.

Pamoja na Mradi na Maji Mayoka- Minjingu Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa pia alitembelea miradi ya Maji katika Kijiji cha Endakiso na Mutuka Wilayani Babati.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.