• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Mnyeti azindua Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama Manyara

Imechapishwa Tarehe: April 11th, 2019

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema ili kuweza kuhakikisha mama mjamzito na mtoto wanakuwa salama ni lazima familia,jamii,taasisi za dini,wadau wa maendeo na serikali ziweke na kuongeza juhudi katika kudhibiti vifo hivyo.

Amesema ili kufanikisha hilo lazima kuwepo mikakati madhubuti katika kusimamia utekelezaji wake ili kuweza kuhakikisha hilo linafanikiwa.

Mnyeti ameyasema hayo wakati akizungumza na wakuu wa wilaya,wakurugenzi,madaktari,wauguzi na wadau mbalimbali wa fya mkoani hapa kwenye uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama”  ambayo Kitaifa ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Oktoba 7,2018 jijini Dodoma.

Amesema katika mkoa wa Manyara hataki kusikia Mama mjamzito anatozwa pesa  anapokwenda kupata huduma au kujifungua kwa kuwa serikali imeshatoa maagizo kuwa huduma hizo ni bure huku akimtaka mganga mkuu  kuanza kuwawajibisha wanaofanya hivyo pomoja na kuwachukulia hatua  madaktari na wauguzi wanaozembea kufanya kazi hali inayopelekea wagonjwa wengi haswa wakinamama wajawazito na watoto kupoteza maisha pindi wanapofika hospitalini kujifungua.

Kampeni hiyo maalum inaongozwa na ujumbe usemao “Jiongeze tuwavushe Salama,Kila mmoja wetu ana wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto.Maneno sasa basi,Sasa Vitendo”.

Aidha ameingia mikataba ya makubaliano na  wakuu wa wilaya juu ya kutekeleza maazimio yote katika maeneo yao na kuhakikisha kampeni hiyo inatekelezwa ipasavyo katika ngazi zote kwenye maeneo yao.

Katika hatua nyingine Mnyeti amesema,mkoa wa Manyara umepokea shilingi Bilioni 6.9 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya katika wilaya ya Mbulu na ukarabati wa vituo tisa vya afya Vya Sunya wilaya ya Kiteto,Dongobesh,Daudi na Tlawi katika wilaya ya Mbulu,Magugu na Nkaiti za wilaya ya Babati,Simbay na Hilbadaw za Hanang pamoja na Orkesumet wilaya ya Simanjiro.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.