Mwenge wa Uhuru umepokelewa kwa shangwe na nderemo Mkoani Manyara ukitokea Mkoa wa Arusha siku ya Jumatano Septemba 19 2018 katika Kijiji cha Minjingu na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexander Mnyeti. Mara baada ya kukabidhiwa Mwenge huo Mkuu wa Mkoa wa Manyara alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Babati Mh.Elizabeth Kitundu ili kuanza kukimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati.
Mwenge wa Uhuru Mkoani Manyara utakimbizwa katika Halmashauri zake zote saba zilizopo Mkoani humo na hatimaye kukabidhiwa Mkoni Kilimanjaro Tarehe 26 Septemba, 2018.
(Kwa Picha mbalimbali za matukio ya Mwenge angalia kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha).
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.