• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ATOA AGIZO KUHUSU WANAFUNZI WANAOMALIZA DARASA LA SABA

Imechapishwa Tarehe: October 9th, 2018


Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amewataka viongozi  katika ngazi ya  mkoa hadi vijiji kote nchini  kuhakikisha wanafunzi  wanaomaliza darasa la saba hawaondoki katika maeneo yao  kwenda kufanya kazi za ndani wakati wakisubiri matokeo ya kuhitimu darasa la saba kwani kwa kufanya hivyo  kunawaondolea fursa yao ya kuendelea na masomo pindi wanapofaulu.  

Naibu waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Manyara wakati akizungumza na viongozi hao kuhusu hali ya Elimu mkoani humo ambapo amewataka kusimamia kwa ukaribu suala hilo ili kutokatisha ndoto za watoto hao na kwamba wale wanaofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

"Hakikisheni watoto hawa wanaposubiri matokeo hawasafirishwi kwani wanapofika huko wanarubuniwa na waajiri hivyo hata matokeo yakitoka na kuonesha wamefaulu hawarejei kuendelea na masomo." Alisisitiza Naibu waziri Ole Nasha

 Amesema fursa za Elimu katika nchi yetu ni kubwa kwa sasa kwa kuwa Elimu msingi ni bure hivyo hakuna kisingizio tena kuwa mtoto hawezi kusoma kwa kuwa mzazi hana fedha

"wazazi msiwe sehemu ya kuchangia watoto wenu kwenda mjini kwa kuwa tu wanawatumia fedha kwa ajili ya matuzi bali hakikisheni mnawasimamia watoto hao katika kipindi chote wanachosubiri matokeo na kuwapeleka shule pindi matokeo yanapotoka na kuonekana wamefaulu,"aliongeza Naibu waziri Ole Nasha

Amewataka viongozi hao kutumia sheria kuhakikisha watoto wenye umri wa kuandikishwa wanaandikishwa  ili kutokuwa na wimbi kubwa la watoto wa mitaani wasioenda shule.

Awali Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Arnold Msuya alimweleza Naibu waziri wa Elimu kuwa mkoa huo una mwamko mdogo wa Elimu  hasa katika jamii ya wafugaji hali   inayopekea kutowaandikisha shule watoto wao wenye umri wa kuanza shule.

Naibu waziri Ole Nasha pia ametembelea  Chuo cha Ufundi stadi VETA Manyara na kuwataka kupitia mitaala yao ili iendane na wakati, ikidhi mahitaji ya soko lakini pia wanafunzi weweze kusoma vitu vingi kwa wakati mmoja na viwe ni vile vinavyoendana  na soko la ajira ili kuongeza fursa ya vijana kujiajiri pindi wanapomaliza masomo yao.

(Kwa Picha mbalimbli na Video za matukio angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha na Maktaba ya Video)

Imeandikwa Na: Haji Athumani (Afisa Habari Mkoa wa Manyara)

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.