• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Naibu Waziri wa Afya atembelea Hospitali ya Rufaa Manyara.

Imechapishwa Tarehe: August 6th, 2020

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Godwin Mollel  jana  August 5 amefanya ziara ya siku moja Mkoani Manyara kwa kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara na kujionea shughuli mbalimbali,kuona jinsi jinsi wagonjwa wanavyopata huduma na kuongea na watumishi wa Hospitali ili kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kazi zao za kila siku katika Hospitali hiyo.

Kabla ya kutembelea Hospitali ya Rufaa Naibu waziri huyo alipokelewa na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti  katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kisha kuendelea na ratiba yake katika Hopitali ya rufaa akiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa  wa Manyara Dkt.Damas Kayera.

Akimkaribisha Hospitalini hapo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt. Catherine Magali alisema kuwa Hospitali inahudumia wastani wa  wagonjwa wa nje 2905 kwa mwezi na wagonjwa wa kulazwa wastani wa wagonjwa 450 kwa mwezi. Pia kutokana na Mkoa kupakana na Mikoa ya Singida na Dodoma Hospitali inahudumia wagonjwa wa kutoka Wilaya za jirani za mikoa hiyo.

“Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara vilevile imekuwa na utaratibu wa kufanya huduma za kibingwa kwa mwaka mara mbili kwa kuita madakatari bingwa waliopo Mikoa ya jirani kwa kushirikiana na madaktari bingwa waliopo hapa ili kufikisha huduma kwa wananchi wenye uhitaji wa Mkoa wa Manyara na Mikoa ya jirani” Alisema Dkt. Catherine.

Akizungumzia juu ya Hospitali kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA Dkt Catherine amesema kuwa Hospitali inatumia mifumo yote kama AFYA CARE, Mfumo wa Maabara (LABNET), Mfumo wa taarifa za kiutumishi (HRHIS),Mfumo wa kusajili watumishi (Biometric register), Mfumo wa GePG kwa ajii ya kukusanya mapatao pamoja na kufunga CCTV Camera kwa ajili ya usalama wa watumishi,mali za Serikai,wagonjwa na wageni wanaoingia na kutoka eneo la Hospitali.

Mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mganga Mfawidhi  Naibu Waziri wa Afya  Mhe. Dkt.Mollel alitembelea kituo maalumu cha kuhifadhia wagonjwa wa Covid 19 na kupewa maelezo kuwa kwa sasa hakuna mgonjwa hata mmoja katika kituo hicho kwani wagonjwa wote wamepona na kuruhusiwa.

Vilevile alitembelea Maabara ya kisasa iliyopo katika Hospitali hiyo na kuona jinsi watumishi wa maabara wanavyofanya kazi  kwa bidii ili kutoa majibu vipimo vyote kwa wakati na kutembelea chumba cha upasuaji, pia alipata nafasi ya kuonana na baadhi ya wagonjwa waliokuja kupata huduma Hospitani hapo na wagonjwa hao kumweleza Mhe. Naibu Waziri wa Afya kuwa wanaridhika na huduma zinazotolewa Hospotalini hapo.

Baada ya kutembea na kujionea shughuli mbalimbali katika Hospitali hiyo Mhe.Naibu Waziri wa Afya alifanya kikao na Watumishi Hospitalini hapo na kusiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo fursa ya kwenda kusoma,punguzo la riba kwenye mikopo.

Dkt.Mollel aliwatoa wasiwasi watumishi hao kwa kuwaeleza kuwa serikali itahakikisha watumishi wote wa Sekta ya Afya na sekta nyingine wanapata stahiki zao kwa mujibu wa miongozo ya serikiali na kuwaasa watumishi kuishi kwa kupendana ili kuwapa huduma bora wananchi.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara ilianzishwa Mwaka 2013 ikiwa chini ya Katibu Tawala Mkoa wa Manyara na baada ya hapo kuanzia mwaka 2018 ilihamishiwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, wazee na Watoto chini ya Katibu Mkuu kutokana na maelekezo kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.