• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

NANE- NANE KANDA YA KASKAZINI YAFANA

Imechapishwa Tarehe: August 6th, 2019

Maonesho ya  kilimo na Wafugaji Kanda ya Kaskazini yanayofanyika Mkoani Arusha katika viwanja vya Themi  yamevutia watu wengi sana wa mikoa ya Manyara ,Arusha na Kilimanjaro kutokana na wafugaji,wakulima na wafanyabiashara mbalimbali kujitokeza katika maonesho hayo na kuonesha bkidhaa zao kwa wananchi.

Akikagua mabanda ya Kilimo Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mh. Iddi Hassani Kimanta alifurahia maonesho hayo na kuzitaka Halmashauri zote katika Kanda ya Kaskazini kulete wakulima na wafugaji kwenye maonesho hayo ili kujifunza mambo mbalimbali na kupeleka ujuzi watakaoupata kwenye jamii wanazoishi ili kujikwamua na umaskini.

“Nimevutiwa sana na jinsi Halmashauri ya Wilaya ya Moshi walivyoanzisha Kilimo cha Vannila kwani kinaongeza kipato sana na pia unaweza kupanda mazao zaidi ya moja kwenye shamba moja kwa mfano Migomba au Kahawa na Vannila” Alisiistiza  Mh.Kimanta

Pamoja na kuvutiwa na Ukulima wa wa Vannila pia aliona jinsi Halmshauri hiyo ilivyowafundisha wakulima wake kutumia eneo dogo kupanada mazao ya mbogamboga  mengi na kuongeza kipato cha familia “Hii unaweza kupanda mboga katika sehemu ndogo ukapata mboga ya nyumbani, ukafanya biashara na pia ikawa ni sehemu ya Bustani kwa ajili ya kupamba Nyumba” Aliongeza Mkuu wa Wilaya ya Monduli.

Pamoja na kuonan shughuli hizo pia aliona jinsi ya uvunaji, usindikaji na upakiaji wa  asali unavyofanyika katika njia bora na kuliongezea thamani zao la asali kwenye Banda la Waziri Mkuu Msaatafu Mh.Mizengo Pinda na kuwataka wafugaji na wasindikaji wengine   wa asali waende wakijifunze kupitia banda hilo.

Vilevile Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli alijionea jinsi wajasiriamali  Vijana kutoka Wilaya ya  Mwanga Mkoani Kilimanjaro walivyoeweza kutumia mbinu rahisi ya ufinyangaji wa vyungu na Wasusi kutoka Halmashauri ya Mji Mbulu wanavyotumia malighafi zilizopo katika maeneo yao kutengeneza mikeka inayodumu kwa muda  mrefu bila kuchafua mazingira.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Monduli alitembelea mabanda ya Kusindika Asali kutoka Katavi kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Pinda,Panda la World Vision, mabanda ya Kilimo kutoka Halmashauri za Moshi Wilaya,Mwanga,Same,Rombo,Longido,Mbulu Mji na Monduli.

Wakijumuisha maonesho kwa siku ya Jana Wakuu wa Wilaya ya Monduli,Same na Monduli waliishauri kamati ya Maandali kutenga siku maalumu kwa kila Mkoa iliyomo  kanda ya Kaskazini kuja kuonesha mambo mbalimbali ya kiutamaduni yanayofanywa katika mikoa yao.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandali ya Nane Nane Kanda ya Kaskazini Anza-Amen Ndossa alisema kuwa watayafanyia kazi yale yote yaliyopendekezwa na kutolewa ushauri na wageni waliotembelea Manoneshoi hayo kwa siku ya jana na siku zote ili kuboresha zaidi msimu ujao. 

   (Kwa picha mbalimbali angalia sehemu ya  Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.