• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

RC Manyara aagiza watumishi wa Idara ya Elimu waliokaa zaidi ya miaka 5 kuhamishwa

Imechapishwa Tarehe: December 16th, 2020

Na: Mariam Juma,Hanang.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti amemwagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Hanang Solomon Isack  kuwahamisha watumishi wa idara ya elimu wilayani hapo waliodumu kwa zaidi ya miaka 5 kwa kile alichokieleza kuwa hao ndio wanaokwamisha jitihada za ufalu wa watoto wilayani hapo.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa inakuja mara baada ya wilaya hiyo kushika nafasi ya mwisho kimkoa  kwa muda wa miaka mitatu  mfululizo  huku watumishi wa idara hiyo wakishindwa kubuni mbinu mpya za kuongeza ufaulu katika wilaya  

“Nimekuja wilaya hii kama Mkuu wa wilaya hii nikakuta Hanang ni ya mwisho watumishi wa idara hiyo  ni wale wale,mwaka wa pili nikiwa hapa tumefeli kama wilaya tena nikiangalia wataalamu waliopo  bado ni wale wale,mwaka huu tena mmefeli watu ni wale wale nasema  Mkurugezi hamisha watu hawa”alisema  Mkirikiti,

Alisema ili kuhakikisha wanaongeza kiwango cha ufaulu wilayani hapo bila kuwahamisha wataalamu hao wa muda mrefu bado ni tatizo kwani hata wakiwaleta Mafisa elimu wengine wapya bila wataalamu hao wa chini yake kuhamishwa bado itakuwa ni tatizo hivyo kinachotakiwa ni kuwahamisha  na kuleta wengine wapya watakaoisaidia wilaya hiyo  kuongeza ufaulu na kuacha kushika nafasi ya mwisho  Kimkoa kila mara.

Mkirikiti akawataka pia kuhakikisha wanakamilisha miundo mbinu ya madarasa  ili wanafunzi waliofaulu waweze kuingia darasani na kuanza masomo yao.

“Mwanzoni mpaka naondoka hapa tulikuwa na upungufu wa madarasa 78 tukayapunguza yakafika 15 sasa kama yameongezeka nendeni hivyo hivyo  msijipunguzie maana kule mkoani  nikiwaambia nileteeni upungufu wa madarasa mnaniambia hamna upungufu wa madarasa  na mnaupungufu wa madarasa 14 lakini mnatakiwa mjiwekee  lengo la madarasa 30 kwasababu mnasema madarasa yanatosheleza Hanang ni kwasababu mmeendelea kuwa watu wa kufeli,hivyo  kwasababu hakuna wakufaulu madarasa ndio maana yanatosha  na kama wangekuwepo kugekuwa na uhitaji”alsema Mkirikiti.

Pia akamtaka Mkurugenzi  kuwahamisha walimu ambao wamekuwa ni wasemaji wa walimu wenzao na wanaofanya kazi kwa mazoea kwani nao hao ni tatizo na wakwamishaji wa elimu wilayani hapo.

Naye Mkuu wa wilaya hiyo  Gharibu  Lingo alieleza kuwa jumla ya watoto  wa darasa la saba waliofaulu  kujiunga na kidato cha kwanza ni 4773 na wanaupungufu wa madawati 1837 pamoja na upungufu wa madarasa 30 na yanatakiwa yapatikane ifikapo January 2021.

Mkuu wa wilaya akawataka madiwani wapya walioapishwa kurudi na kujua mikakati ya kumaliza mapungufu  hayo kwa kuwa mikakati ya awali ni kuhakikisha watoto waote waliofaulu  wanaingia madarasani

“Madiwani rudini kwenye  kamati zenu  za maendeleo za kata Ili mkaweke mipango mikakati mtakayokuta wajumbe wenu wameiandaa lakini pia mboreshe na mtakapokwama tuwasiline maana sisi ni wamoja “alisema Lingo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.