• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

RC SENDIGA AKABIDHI PIKIPIKI 66 KWA JUMUIYA ZA MAJI RUWASA

Imechapishwa Tarehe: January 23rd, 2024

Na Mwandishi wetu - Mjini Babati

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amekabidhi pikipiki 42 kwa awamu ya Pili kwa jumuiya za watoa huduma za maji katika wilaya zote za Mkoa wa Manyara ambapo awamu ya kwanza ziligawiwa pikipiki 22, hii ikiwa ni kurahisisha utendaji kazi kwa watumiaji hao. Pikipiki hizo zimetolewa na Wakala wa Maji Safi na Salama na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Manyara.

Pikipiki hizo zimetolewa na Wakala wa Maji Safi na Salama na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Manyara. Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Mhe. Sendiga amesema ni vyema kwa watumishi hao kuzitunza kwani ni mali ya serikali.

"Niwasihi tukahakikishe pikipiki hizi zinaenda kutumika kama ilivyokusudiwa na kuhakikisha skimu za maji zinakuwa endelevu na Wananchi wanapata huduma ya maji muda wote kwani ni haki yao ya msingi",  amesema Mhe. Sendiga.

Aidha, Mhe. Sendiga amewataka wakuu wa taasisi mbali mbali kukusanya fedha za Umma kwa uadilifu kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zilizopo na kusitokee chombo chochote kukiuka kwa sababu yoyote huku akiwasihi wakuu wa wilaya wote kuendelea kusimamia vyema uhai wa miradi iliyojengwa.

"Serikali imewekeza fedha nyingi sana kujenga miradi hii ya maji, fedha hizi ni zenu kupitia kodi na tozo mbalimbali, tunajukumu kubwa la kuitunza miradi ili kuhakikisha kusudi la Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan la kumtua mama ndoo kichwani linafikiwa", amesema Mhe. Sendiga.

Akitoa shukrani zake kwa RUWASA Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema amesema kuwa atasimamia na kufuatilia kwa Ukaribu kama watumisji waliokabidhiwa pikipiki hizo wanazifanyi kazi kama ambavyo kusudio la Serikali ilivyowaagiza.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA mkoa wa Manyara Injinia Wolter Kilter amesema lengo la kuwapa pikipiki hizo kwa watumiaji hao ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za maji kwa uharaha zaidi.

Amesema kuwa Mkoa wa Manyara unajumla ya Vyombo 88 vinavyosimamia Skimu za maji 346 na kuhudumia wananchi 1,268,239 ambapo mpaka Septemba 30, 2023 zilikusanywa jumla ya Tshs 2,113,232,529", amesema Injinia Kilter.

Ameongeza kuwa RUWASA inaendelea kuvipatia mafunzo jumuiya za watumiaji Maji kama jinsi ya kuandaa mpango wa biashara na ufungaji wa hesabu, vyombo 32 vimeshapatiwa mafunzo hayo mpaka Julai 23, 2023.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.