Mkuu wa mkoa wa manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amezindua Kliniki maalumu ya Madaktari Bingwa wa ndani ya Mkoa wapatao Kumi na tano (15). Kliniki hiyo imezinduliwa leo katika wilaya ya Simanjiro ikiwa na lengo la kutoa huduma bobezi za matibabu kwa wananchi wa Wilaya zote tano (5) za Mkoa Manyara.
Akizindua Kliniki hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, amesema zoezi la utoaji huduma litadumu kwa siku tano (5) katika Hospitali ya Wilaya ya Simanjiro.
RC Sendiga, ameelezwa kua kwenye Kliniki hiyo ambayo itakuwa inafanyika kila baada ya miezi mitatu itahusisha utoaji huduma za magonjwa ya kinamama na watoto, shinikizo la damu la juu, kisukari, Magonjwa ya Macho na magonjwa mengineyo na kuwapunguzia wananchi gharama za kufata matibabu hayo meeneo ya mbali ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akiwatuma mikoani Madaktari Bingwa wa Samia kutoa huduma mbalimbali za kitabibu.
Sambamba na hilo RC, amekabidhi pikipiki nne (4) na viti mwendo sita (6) vya wagonjwa kwa ajili ya kusaidia na kurahisha huduma kwa watumishi wa idara ya afya katika vijiji vya lolipande, Ruvu Remiti, Kitwai na Mwajanga.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.