Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga leo Agosti 14, 2024, ametembelea Shule mpya ya wasichana Manyara Girls na kuongea na wanafunzi pamoja na kuwakaribisha rasmi Mkoa wa Manyara wanafunzi 110 waliokwishawasili shuleni hapo na kuanza masomo yao ya kidato cha tano (5) kwa mchepuo wa Sayansi (PCM na PCB).
Mhe. Mkuu wa Mkoa, amewashukuru na kuwapongeza wazazi walioleta watoto wao katika shule hiyo mpya na kuwahakikishia kuwa watoto wao watapata Elimu na huduma bora, ulinzi na usalama wakati wote watakapo kuwepo shuleni hapo.
Sambaba na hilo RC Sendiga, ameagiza umaliziaji wa miundombinu yote ambayo bado haijakamilika ikamilike mapema ili wanafunzi waweze kupata huduma hizo hasa ya bwalo.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.