• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

SERIKALI HAITABOMOA NYUMBA ZA WATU WALIOJENGA KATIKA MAKAZI HOLELA

Imechapishwa Tarehe: January 14th, 2019

Waziri wa aridhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Lukuvi amesema kwamba Serikali ya awamu ya tano kuanzia sasa haitabomoa tena numba za wananchi waliojenga maeneo ya makazi yasiyo rasmi badala yake itarasimisha makazi holela.

Waziri Lukuvi amesema Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametoa fursa kwa wananchi wote maskini waishio mijini  waliojenga bila kufuata mipango miji na hawana hatimiliki za ardhi kufanyiwa urasimishaji wa makazi yao na wasibomolewe nyumba zao tena kwa kuwa haikuwa makosa yao kujenga maeneo hayo.

Lukuvi ameyasema hayo alipokuwa Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara alipofanya ziara yake ya kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi kwa wakazi wa Mji huo,ambapo amesema wananchi wote wachangamkie fursa hiyo iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli ya kuwapa fursa ya kumiliki hati katika maeneo ambayo siyo rasmi kwa kurasimishiwa.

“Serikali ya awamu ya tano inajali sana wananchi wake kwa kuwa zamani wananchi ambao hawakujenga kwa kufuata mipango miji wangebomolewa nyumba zao, lakini kwa sasa Serikali ya awamu ya tano imeanzisha mpango wa kurasimisha makazi holela na kuwatia hati wananchi wote waishio mijini ili waishi katika makazi rasmi”Amesema Mh.Lukuvi

Aidha Lukuvi amewataka wananchi wote waishio mijini kuwa wazalendo kwa kurasimisha maeneo  yao waweze kujipatia hati na ili walipe kodi ya pango la ardhi jambo ambalo litaingezea Serikali mapato.

Lukuvi apokuwa ziarani Simanjiro mwishoni mwa wiki aligundua kuwa wakazi wa mji wa Simanjiro walio na hatimiliki za ardhi hawazidi 1000 wakati nyumba zilizopo ni nyingi zaidi ya idadi hiyo,hivyo Waziri Lukuvi akawataka wachangamkie fursaa hiyo ya kujipatia ili kuzipa hadhi nyumba zao.

“Nyumba isiyokuwa na hati haina thamani kwa kuwa hata ukienda Benki kukopa pesa hawatakuuliza umejenga nyumba ya uzuri gani,lakini watakachotaka ni hati yako ya kumiliki ardhi ambacho ndio kitu kilicho na thamani zaidi kwako kuw nacho” Aliongeza Lukuvi.

Naye Mbunge wa Simanjiro Mheshiwa James Ole Millya amemshukuru Mheshimiwa Lukuvi pamoja na Serikali ya awamu ya tano katika kuwajali wananchi wake kwa kuwaletea maendeleo makubwa na kusimamia suala la wananchi wa kawaida kupata fursa ya kumiliki ardhi kutoka kwa wawekezaji wakubwa ambao walikuwa hawayaendelezi mashamba yao kwa muda mrefu.

Simanjiro ndio wilaya inayoongoza kwa wamiliki wa mashamba makubwa walio na hati na hata wengine wasio na hati rasmi.Kwa sasa mashamba makubwa yasiyo na hati rasmi yanafika 158 yaliyo na jumla ya ekari zaidi 120,000 ambapo wasio na hati ni zaidi ya hao, hivyo Waziri ameanza utaratibu wa kufuta mashamba makubwa 55 wilayani humo yanayomilikiwa  kwa kuwa wamiliki wake wamekiuka masharti ya umiliki.  

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.