• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

SERIKALI KUAJIRI WALIMU 6000 MWAKA HUU

Imechapishwa Tarehe: January 22nd, 2019

Serikali imesema kuwa mwaka huu inatarajia kuajiri walimu wapya 6000 wa masomo ya Sayansi na Hesabu ambapo tayari kibali cha kuwaajiri walimu hao kimekwishatolewa.

Aidha Serikali inakusudia kuwapeleka walimu 11,000 wa masomo ya sanaa ambao ni wa ziada waliokuwa wakifundisha shule za sekondari kufundisha shule za msingi ili kukabiliana na upungufu wa walimu unaozikabili shule za msingi nchini.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe.Mwita Waitara ameyasema hayo juzi tarehe 20/01/2019 katika Wilaya Chemba, mkoani Dodoma wakati akizungumza na watumishi kutoka Idara za Elimu ya Msingi na Sekondari kutoka Halmashauri hiyo.

Kauli hiyo ya Serikali inafuatia taarifa ya Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Chemba bwana Josephat Ambilikile kumweleza Naibu Waziri kuwa Halmashauri ya Chemba ina upungufu wa walimu 808 kati ya walimu 1628 wanaotakiwa kufundisha katika shule za msingi 103 zilizopo katika wilaya hiyo.

Mhe.Waitara alisisitiza kuwa Serikali kuanzia mwaka huu itakuwa ikiajiri walimu kila mwaka ili kufidia walimu wanaostaafu na pia kukabiliana na upungufu unaotokana na ongezeko kubwa la wanafunzi katika shule za msingi kutokana na mwitikio wa wazazi kupeleka watoto wao shule kufuatia uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kutoa elimu ya bila malipo.

“Tayari Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli amekubali walimu waajiriwe na kibali kimekwishatolewa hivyo walimu 6000 wa masomo ya sayansi na hesabu na pia walimu 11,000 ambao ni walimu wa ziada waliokuwa wakifundisha masomo ya sanaa katika shule za sekondari watapelekwa kufundisha shule za msingi,” alisema Mhe.Waitara.

Pamoja na kueleza juhudi hizo za serikali za kuongeza idadi ya walimu, Naibu Waziri aliwataka walimu wanaofundisha masomo ya sayansi na hesabu kutowakatisha tamaa wanafunzi wanapowafundisha wanafunzi masomo hayo badala yake watumie mbinu rahisi ili wanafunzi waelewe kwa urahisi masomo hayo.

“Tunatarajia Walimu wanapaswa kutumia mbinu rahisi wanapofundisha hesabu ili wanafunzi wapende somo hilo,” alisema na kuongeza:

“Hata utunzi wa vitabu vya kufundishia masomo hayo inabidi uangaliwe upya kwani watoto wanakimbia kusoma masomo ya sayansi na hesabu kwani kutokana na namna vitabu hivyo vinavyotungwa vinasababisha watoto wachukie masomo ya sayansi na hesabu,” alisema Waitara.

Jambo lingine alilolizungumzia Naibu Waziri ni kiwango duni cha ufaulu kilichoonyeshwa na Mkoa wa Dodoma hasa wilaya ya Chemba katika matokeo ya kitaifa ya darasa la saba na kidato cha nne ambapo aliwataka watendaji wa elimu katika halmashauri hiyo kuja na mikakati itakayoboresha elimu wilayani humo.

“Ukitaja wilaya 10 zilizofanya vibaya kwa ufaulu Chemba ni ya 10 kwa matokeo ya darasa la saba, mkae chini mje na mkakati wa kuboresha matokeo ya wilaya yenu, cha muhimu mikakati hiyo ishirikishe ngazi zote kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya, tarafa hadi kata,” alisema.

Pia Naibu Waziri alikemea tabia iliyojitokeza hivi karibuni kwa baadhi ya watendaji wa elimu kushiriki katika kuiba mitihani ambapo aliagiza kuwa kama kuna mwalimu ameshiriki katika wizi wa mitihani halmashauri isisite kumchukulia hatua kwani kitendo hicho kinarudisha nyuma maendeleo ya elimu ya nchi.

Sambamba na hilo Mhe.Waitara alionya tabia ya baadhi ya watendaji wasio waaminifu katika halmashauri kutumia kinyume na maelekezo ya serikali fedha za miradi kwa ajili ya kusaidia miundombinu ya shule.

“Fedha kama ni kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ipokee na iende ikajenge hosteli, kadhalika kama fedha ni kwa ajili ya kununulia samani za shule ipokee na iende ikanunue samani za shule, ukigusa fedha ya elimu kinyume na maelekezo ya serikali tutashughulika na wewe,” alionya Waitara.

Mapema Naibu Waziri alipata fursa ya kutembelea shule ya sekondari na shule ya msingi ya Chemba na kushuhudia ujenzi unaoendelea wa chumba kimoja cha darasa katika shule ya sekondari chemba, ujenzi ambao umetokana na michango ya wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mheshimiwa Simon Odunga alimweleza Naibu Waziri kuwa  wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa walimu na kukosekana kwa utayari kwa jamii kuchangia masuala ya elimu kwa dhana kuwa kila kitu kinatolewa bure na serikali.

Na Mathew Kwembe, Chemba, Dodoma

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.