• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

SERIKALI KUHIFADHI ZIWA BABATI

Imechapishwa Tarehe: September 7th, 2018

Waziri wa nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Januari Makamba (Mb) alifanya ziara Katika Mkoa wa Manyara na kutembelea Halmashauri ya Mji wa  Babati tarehe 6/9/2018 na kuongea na viongozi pamoja na wananchi juu ya uhifadhi wa ziwa babati. 

Akiongea na viongozi waziri Makamba alisema  "Dhumuni la ziara yangu ni kuhakikisha sifa ya Tanzania  inabaki katika uhifadhi wa rasilimali kwa ajili ya kizazi kijacho na pia ipo fursa ya kuyatunza na kuyahifadhi maeneo yetu lindwa yaliyopendekezwa na Mkoa wenu kwa kutumia sheria ya mazingira”.

Aidha waziri Makamba alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Manyara kuteua kikundi cha maafisa au wataalam wa mazingira ili wakapate mafunzo juu ya uhifadhi wa mazingira ,pia alizitaka Halmashauri kuungana na (NEMC) ili kukasimu kazi zake katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika kukusanya ada kama chanzo cha mapato vilevile alisema huduma za kiikolojia zinaweza kuufanya Mkoa kunufaika na huduma za kiutalii na pia alitoa rai kwa viongozi sheria ndogo za kimazingira zibadiliswe mfano sheria ya ndogo ya Halmashauri ya Mbulu ya uhifadhi wa mazingira ya Mwaka 2004.

Katika mkutano wake na wananchi wa kijji cha Himiti katika Kata ya Bonga Halmashauri ya Mji wa Babati Mh. waziri alisema ziwa Babati lina nafasi kwa ustawi wa maendeleo ya watu wa Babati zipo changamoto zinazolikabili ziwa hilo” ni mezungumza na mwenyekiti wenu kaniambia samaki wamepungua na hii ni kutokana na  kina cha maji kupungua, tope limeongezeka na magugu yanazidi kuota hivyo ikifika miaka kumi na tano litatoweka kabisa” alisisitiza.

Mapendekezo yaliyotolewa na Mkoa wenu ziwa hili lihifadhiwe katika mambo ya kimazingira ni lazima wananchi washirikishwe kama kifungu cha 178 cha sheria ya mazingira kinavyosema “Umma una haki ya kupata taarifa muafaka kuhusu kusudio la mamlaka za kiutawala kuhusu mazingira” ,hivyo basi kila mwananchi ni mdau wa mazingira na ana haki ya kushitaki kwa niaba ya mazingira na maslahi ya watu yatazingatiwa kwa watu wote.

Halikadhalika Mh. Waziri alitoa fursa kwa wananchi kuchangia maoni yao kupima na kutathimini juu ya utayari  wa wananchi katika mpango wa serikali unaolenga kulifanya ziwa Babati kuwa eneo lindwa ambapo wananchi hao walisema ”ziwa hili ni kama ajira kwetu hivyo Mh. Waziri mimi siipingi hoja yako kwani umeileta kwetu kwa ajili ya maslahi yetu hivyo tunakubaliana na hoja ya uhifadhi wa ziwa letu kwani asilimia kubwa ya sisi wa kazi wa hapa kazi zetu ni uvuvi kilimo na ufugaji” alisema Ayubu Gwangway

Kwa sababu mimi mwenyewe kama mkereketwa mmojawapo naunga mkono hoja ya uhifadhi wa mazingira kwani ziwa hili mkiliwekea mikakati madhubuti na sheria za kiuvuvi samaki wataongezeka na sisi kama wananchi tutanufaika kwa kutupatia kipato cha familia kwani kazi zetu sisi ni uloezi wa samaki ambao hutupatia fedha kwa ajili ya kusomeshea watoto wetu” alisisiti za Asha Hussein mkazi wa kijiji hicho.

Vilevile mkazi mwingine alisema sheria zinasaidia kutupeleka kwenye mafanikio kwani uvuvi haramu umekuwa gumzo,kilimo kisicho cha mpangilio kimechangia sana tope kujaa ziwani hivyo suala hili tumelikabidhi kwenu Serikali kwa ajili ya uhafidhi wa ziwa letu kwa ajili ya kuchangia pato la serikali.

Kutokana na maoni hayo ya wananchi Mh.Waziri Makamba alisema ameyapokea maoni hayo kwa mikono miwili hivyo nitayafikisha kwa viongozi wenzangu na nitatuma timu ya wataalam kuja kufanya uchunguzi kuweka mipaka na sheria zitakazowaongoza katika uhifadhi. Akifunga kikao mwenyekiti wa kijiji Cha Himiti wao kama wananchi wanaungana na Serikali katika kulihifadhi ziwa kwa malengo ya Taifa na kizazi kijacho na tuko tayari kutoa ushirikiano kwa watalam na Serikali katika kuyatunza mazingira yanayotuzunguka kwa ujumla pamoja na uhifadhi wa rasilimali tulizonazo.

(Kwa Picha mbalimbali angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)

Imeandikwa na Isabela Joseph (UDSM-Mafunzo kwa Vitendo)


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.