• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

SERIKALI YATOA MAAGIZO MGOGORO WA ARDHI KIRU

Imechapishwa Tarehe: February 13th, 2023

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amemuelekeza Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Manyara kuweka mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi na kuwapatia hati wakazi wa eneo la ekari 2,390 zilizotolewa na Rais katika Bonde la Kiru Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Kikwete ametoa maelekezo hayo kwa Kamishna  Joseph Batinamani wakati alipofanya ziara  Februari 11, 2023 katika kijiji cha Kiru Dick kata ya Kiru, halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, kutokana na mgogoro uliopo kati ya wakazi wa Kijiji cha Kiru Dick  na mwekezaji wa kampuni ya Hamir Estate Ltd inayojishughulisha na kilimo cha miwa ambaye ni wamiliki wa awali wa Mashamba hayo.

Itakumbukwa kwamba  Rais wa  awamu ya Nne wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete aliamua kumega ekari 2,390 ambazo zilikuwa zikimilikiwa kihalali na Kampuni ya Hamir Estate Ltd kwenye mwaka 1999 na kuwapa wananchi ili kumaliza mgogoro huo.

Wananchi hao mpaka sasa bado hawajakabidhiwa maeneo hayo kwa kuwa bado serikali inafanya mazungumzo na mwekezaji huyo kuhusu Fidia ili kuachia maeneo hayo yaende kwa Wananchi.

Aidha Kikwete amewaonya wakazi wa eneo hilo kujiepusha na uvunjifu wa amani kwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu ambavyo vimekuwa vikiendelea katika eneo hilo na badala yake amewataka kuonesha ushirikiano kwa muwekezaji huyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Charles Makongoro Nyerere amewataka wakazi wa eneo hilo kuwa nasubira wakati Serikali ikiendelea na utekelezaji wa maelekezo ya Rais ili wananchi hao waweze kupangwa na kumilikishwa maeneo hayo na kupatiwa hati za umiliki wa ardhi Kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo Wananchi hao walipewa nafasi ya kuzungumza ambapo waliiomba serikali ishughulikie suala Hilo haraka.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete Pamoja na Mkuu wa Mkoa Manyara Charles Makongoro Nyerere walilazimika kuanza kutoa darasa kwa wananchi hao juu ya taratibu zote za Ardhi Kwa zaidi ya saa tatu.

Kutokana na eneo hili kuwa na rutuba sana limevutia wawekezaji wakubwa wengi wa kigeni na wenyeji wachache kwenye shughuli za kilimo hasa kilimo cha miwa toka enzi za Mjerumani na baadae Muingereza pamoja na mataifa mengine kama Urusi, Swedeni, Marekani toka miaka ya 1930.





Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Miaka Miwili ya Rais Samia Manyara ni Shangwe tupu Miradi ya Maendeleo

    March 18, 2023
  • SERIKALI YATOA MAAGIZO MGOGORO WA ARDHI KIRU

    February 13, 2023
  • MITI MILIONI 10.5 KUPANDWA MANYARA

    January 27, 2023
  • RC MAKONGORO AMESEMA WALIOCHAGULIWA WATAINGIA DARASANI BILA USUMBUFU WOWOTE

    January 23, 2023
  • Tazama Zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru 2022 Mkoa wa Manyara
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.