• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

TAMISEMI yaandaa mwongozo mpya wa usimamizi wa mapato kwa Halmashauri

Imechapishwa Tarehe: January 17th, 2019

Serikali imesema kuwa mwongozo mpya wa ukusanyaji mapato katika halmashauri unalenga kuongeza wigo wa makusanyo ya mapato kwa kuwatoza watu wengi badala ya wachache na hivyo kuziwezesha halmashauri kukusanya mapato mengi zaidi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mratibu wa Mradi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Beatrice Njawa mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kujadili Mwongozo wa Usimamizi Ukusanyaji Mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ndogo ya TAMISEMI iliyopo jijini Dar es salaam.

Alieleza kuwa mwongozo wa usimamizi wa mapato utapanua wigo kwa kuwatoza wale wote wanaostahili kutozwa mapato mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushuru na kodi mbalimbali za Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Bi Njawa aliongeza kuwa mwongozo mpya sambamba na kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato ya halmashauri umezingatia kushirikisha maoni ya wadau hususani sekta binafsi ili waweze kutoa elimu kwa wadau wao wa namna bora ya kuutekeleza mwongozo huo ili kufikisha malengo yaliyokusudiwa.

“Kupitia mwongozo huu tumeshirikisha sekta binafsi ambao watatusaidia kutambua baadhi ya  shughuli za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao ili tuweze kuibua vyanzo vipya isipokuwa kwa tahadhari kwamba havitakuwa kero katika jamii ya wafanya biashara.

Mapema akifungua kikao hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam bwana Abubakar Mussa Kunenge alisema kuwa Mwongozo huo ni jitihada za Serikali za kuziwezesha Halmashauri kukusanya Mapato ya Vyanzo vya Ndani kwa ufanisi na kikamilifu. Kadhalika, kuweka mikakati ya kuwezesha kuwepo kwa mazingira wezeshi ya kufanya biashara na uwekezaji.

Aliongeza kuwa mwongozo huo unalenga kuweka utaratibu rahisi wa utambuzi wa Fursa za kiuchumi na Sekta ya uzalishaji, utambuzi wa Walipa kodi, taarifa na takwimu za kodi, namna ya kusimamia na kukusanya mapato, ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika mipango na utekelezaji wa mikakati ya ukusanyaji mapato, kuongeza uwajibikaji na uwazi katika kukusanya na kutumia mapato yaliyokusanywa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais TAMISEMI Bwana Shomari Mukhandi alisema kuwa Ofisi yake imeona ni vyema kukaa na wadau kujadili rasimu ya mwongozo huo ili kupata maoni ya kila mshiriki ili kuboresha Mwongozo wa Ukusanyaji Mapato kulingana na mahitaji ya Sekta mbalimbali za Kiuchumi na Kijamii kwa kuzingatia kuimarisha Uwazi, Uwajibikaji na Ukuzaji  Uchumi.

Naye bwana Donald Ria ambaye ni Mtaalamu Mshauri wa masuala ya mazingira ya biashara na uwekezaji kutoka Mradi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Denmark na Tanzania alisema kuwa mradi wake ulikubali kufadhili kuandaliwa kwa mwongozo huo ili kuboresha ukusanyaji wa mapato katika halmashauri.

Na Mathew Kwembe 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.