• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

TEHAMA KUONGEZA UFANISI KWA WATUMISHI WA AFYA NGAZI YA ZAHANATI

Imechapishwa Tarehe: September 13th, 2018

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi isiyo ya kiserikali ya PATH chini ya Mpango wa kuboresha Matumizi ya Takwimu za Afya (Data Use Partinership -DUP) imejiwekea mikakati ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma ya Afya kwa kuiweka Mifumo ya TEHAMA katika ngazi ya huduma ya Afya ya Msingi ili Wananchi waweze kupata huduma bora za afya.

Akitoa mada katika kikao kazi cha kuimarisha mifumo ya TEHAMA inayotumika katika Ngazi ya vituo vya afya kilichofanyika katika ukumbi wa NIMR, Jijini Dar-es-salaam Bi. Sultana Seif Afisa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto amesema ili kumuwezesha mtumishi wa afya ngazi ya zahanati na kuweza kutoa huduma stahiki ni vyema wakafanya kazi kwa ufanini atika utendaji kazi wa kila siku kwa kutumia TEHAMA.

Bi. Sultana amesema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali katika upatikanaji wa huduma sahihi na upatikanaji wa takwimu sahihi za afya kwa jamii jambo ambalo linapelekea mtumishi wa afya ngazi ya zahanati kuwa na mzigo mkubwa unaopelekea kutojaza takwimu sahihi na kushindwa kuwahudumia wananchi kwa wakati.

Amesema Serikali baada ya kuona changamoto hiyo imejiwekea mikakati ya kumsaidia mtumishi wa ngazi ya zahanati kutumia TEHAMA katika ukusanyaji, utunzaji na utumiaji wa takwimu sahihi katika kufanya maamuzi.

 “Imekuwa ni utaratibu wa Mtumishi wa afya ngazi ya nchini kuwa na fomu nyingi za kujaza (mfano mtua) hivyo serikali iliamua kuingiza mifumo ya TEHAMA ambayo itakusanya taarifa zote na kuwa moja ili kumuwezesha mdau kuweza kupata takwimu zilizosahihi na kwa wakati za mgonjwa na mahitaji muhimu katika utoaji wa huduma” anasema Sultana.

Amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuwawezesha wadau kutoa changamoto zilizopo katika utoaji wa huduma katika ngazi ya Msingi ya utoaji huduma na kupendekeza jinsi ya kuboresha utoaji wa huduma za afya na kupunguza mizigo kwa watumishi.

Amesema kuwa kwa sasa serikali inampango wa kutoka katika matumizi ya karatasi na  kuingia katika matumizi ya TEHAMA hivyo kunatakiwa kuwa na Dira itakayosaidia kuonyesha muelekeo katika kufanya mabadiliko ya TEHAMA kwenye kutoa huduma za afya nchini

Aidha  amesema kuwa lengo kuu ni utoaji wa huduma bora kwa jamii, kuwa na takwimu sahihi na kwa wakati na kuingia katika mifumo ya TEHAMA  kutoa huduma sahihi na upatikanaji wa takwimu sahihi.

“Unakuta mtumishi wa afya katika ngazi ya Zahanati anahudumia mteja huku ukijaza fomu mbalimbali kwa ajili ya kuweka rekodi jambo ambalo linasababisha kutokuwa makini na ujazaji wa takwimu na kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi.

Aidha amesema kuwa Mifumo ya TEHAMA itasaidia utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati , upatikanaji wa taarifa ya mgonjwa popote pale nchini kwa urahisi.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii, Idara ya afya, Ustawi wa Jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Rasheed Maftah amesema kwa sasa TAMISEMI ipo katika hatua ya kuboresha huduma za afya ya msingi kwenye Mamlaka za Serikali za mitaa.

Anafafanua zaidi na kusema kuwa moja ya hatua ya msingi ni  kuimarisha huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati kwa kuimarisha mifumo ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa jamii.

Bw. Maftaa amesema kuwa Mpango wa kuboresha Matumizi ya Takwimu za Afya (Data Use Partinership –DUP)ulianza na mchakato wa kupata maeneo ya  kimkakati ya uwekezaji na baada  ya kupatikana ndipo utekelezaji ulipoanza ambapo kwa sasa upo katika hatua ya awali ya utekelezaji.

Aidha amesema sema Mpango huo utasaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuongeza ufanisi na  ubora wa utoaji huduma kwa wananchi hususani katika Zahanati na vituo vya afya,  kuboresha miundombinu ya TEHAMA, kuawajengea uwezo watumishi  na kubadilisha mifumo ya awali iliyokuwa ikifanyika kwa njia ya karatasi  na kuingiza mifumo hiyo katika TEHAMA.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.