Wafungwa 207 wameachiwa huru Mkoani Manyara kati ya wafungwa 5533 waliochiwa huru na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alioutoa katika maadhimisho ya kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika Mkoani Mwanza.
Akizungumza na wafungwa hao siku ya jumanne tarehe 10/12/2019 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexander Mnyeti amewataka kutumia fursa hiyo kuwa watu wema katika jamii .
“Mmepewa msamaha na Mheshimiwa Rais jana, sasa sitegemei kusikia keshokutwa mmerudishwa tena magereza kwa kufanya makosa, mkifika uraiani muwe watu wema na sio kufanya uhalifu kwa mara nyingine” Alisema Mkuu wa Mkoa.
Afisa Magereza Mkoa wa Manyara Lipina Lymo amesema kati ya wafungwa hao 141 walikuwa gereza la Babati mjini, 21 gereza la Kiteto, 45 gereza la Mbulu.
Amesema walioachiwa huru ni waliokuwa na makosa madogo na waliobakiza siku chache kumaliza vifungo vyao kuanzia siku moja hadi miezi kumi na mbili.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.