• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Wakurugenzi zingatieni miongozo ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma

Imechapishwa Tarehe: January 31st, 2019

Serikali imewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha za serikali ili kupunguza matumizi mabaya ya fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya Elimu.

Akifunga mafunzo elekezi kuhusu utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo katika Sekta ya Elimu (EP4R) jana jijini Dodoma, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya)  Mhe. Josephat Sinkamba Kandege alisema kuwa serikali itahakikisha kuwa hakuna shilingi hata moja itakayopotea wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha kuwa fedha yote itakayotolewa kwa ajili ya miradi inayopelekwa halmashauri ama iwe imetoka serikalini au kwa wahisani haitumiki kinyume na malengo yaliyokusudiwa

“Kila shilingi tunataka iwe na tija, hivyo nawataka wakurugenzi wa halmashauri na watendaji wengine mhakikishe kuwa mnafuata miongozo ili muepuke hoja za ukaguzi,” alisema

Aliongeza kuwa kila kiongozi  anatakiwa  kufanya kazi kwa weledi  na kuacha tabia ya kufanyakazi kwa mazoea na kuzingatia  miongozo na maelekezo  ya matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali  pamoja na wadau wa maendeleo  ili kuepuka hoja za wakaguzi.

Pia aliwaagiza watendaji hao kusimamia  na  kufatilia utekelezaji wa miradi hasa ujenzi wa miundombinu ya shule ili ikamilike kwa wakati  na kuwashirikisha  kamati, bodi na jamii inayozuguka  katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na  kupunguza ghalama zisizoza msingi, kutoa ajira kwa jamii husika na kuharakisha katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Alisema matumizi ya fedha yanayotumika katika miradi husika yaendane na thamani ya mradi husika ili kuhakikisha sekta ya elimu inapata matokeo chanya.

Aidha Mhe. Kandege alisema ili kuthibiti ubora wa elimu nchini halmashauri  zihakikishe shule zinakaguliwa kwa wakati  muafaka na changamoto zinazobainishwa na wathibiti ubora zifanyiwe kazi haraka ili watoto wa kitanzania wapate elimu bora.

“Wakaguzi wa Halmashauri toeni ushirikiano kwa wathibiti Ubora wa Elimu na Mafunzo elekezi kwa wakuu wa shule juu ya umuhimu wa kutekeleza ukaguzi wa ndani ya shule pale panapo kuwa na changamoto mawasiliano  yafanyike kwa wakati kupitia  Ofisi ya Mkoa ili  muweze kufikia malengo ya pamoja,” alisema.

Mapema kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri kufunga kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa  Elimu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu ya Msingi Dkt. George Jidamva alisema changamoto kubwa waliyoiona kwenye utekelezaji wa mradi huo ni kwa baadhi ya watendaji kushindwa kujibu hoja za ukaguzi kwa kukosa vielelezo muhimu kama risiti na orodha ya malipo.

Changamoto nyingine ni kutofautiana kwa ubora wa majengo kati ya halmashauri na halmashauri licha ya kuwa ramani za miundombinu hiyo kufanana na hivyo kukosekana kwa thamani ya ubora kutokana na baadhi ya majengo kujengwa chini ya kiwango.

Mradi lipa kulingana na matokeo katika sekta ya elimu ( EP4R) ulianza Septemba, 2014 kwenye Mamlaka za serikali za mitaa kwa kupokea kiasi cha shilling bilioni 77.98 na kwa sasa halmashauri hizo zinatarajia kupokea kiasi cha shilling biloni 40 kutoka kwa wadau wa maendeleo ambazo zitatumika  kwa mujibu wa maelekezo yatakayo tolewa na mamlaka husika.

Na: Majid Abdulkarim na Mathew Kwembe

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.