• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

WAKUU WA WILAYA WATAKIWA KUSOMA SHERIA NA TARATIBU

Imechapishwa Tarehe: August 15th, 2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa hivi karibuni kuhakikisha wanasoma na kuzielewa sheria zinazowaongoza ili kufanya kazi kwa weledi.

Mhe. Jafo aliyasema  hayo jana Jijini Dodoma kwenye kikao kazi na Wakuu hao wa wilaya kwa lengo la kuwapa maelekezo ya kazi ambapo aliwaambia mada kuu ya kikao hicho ni mahusiano na mawasiliano kazini pamoja na kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

“Msiende kuwa vyanzo vya migogoro kwenye Wilaya zenu, tumekuwa tukishuhudia migogoro baina ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri, Makatibu Tawala pamoja na Wabunge, hatuwezi kwenda hivi, katengenezeni serikali” Alisema Waziri Jafo.

Hata hivyo alikemea tabia ya baadhi ya Wakuu wa Wilaya kuyatumia vibaya mamlaka waliyonayo na kuwaweka watu ndani hali iliyopelekea wananchi kuichukia serikali yao, hivyo kuwataka kutumia sheria kama iliyokusudiwa na siyo kwa kuonea watu.

Aidha aliwataka Wakuu hao wapya wa Wilaya kutoa ushirikiano kwa wale wanaotekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na siyo vinginevyo ikiwa ni pamoja kusimamia miradi ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya afya na elimu unaoendelea kote nchini.

Kwa upande mwingine Waziri Jafo amesema “Kasimamieni ukusanyaji wa mapato ya serikali kupitia mfumo wa kieletroniki sambamba na kudhibiti uvujaji wa mapato hayo, lakini pia mkadhibiti madeni kwa kuwa fedha hizo ndizo zinazotegemewa kwa ajili ya maendeleo nchini”

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Injinia Mussa Iyombe amewataka Wakuu hao wa wilaya kuzitendea haki nafasi walizopewa kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zilizopo hasa pale wanapomuadhibu mtumishi aliyekosea.

“Serikali ina taratibu zake, baadhi ya wakuu wa wilaya walikuwa wanatia aibu, kama kuna mtumishi kakosea, tumia mamlaka zinazomuongoza kumshughulikia, na sio kusimamisha watu kazi hovyo, kutumbua tumbua hovyo” Alisisitiza Injinia Iyombe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro kwa niaba ya wakuu wenzake wa wilaya amesema watahakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

Imeandikwa na: Haji A.Msovu (Afisa Habari Mkoa wa Manyara)  

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.