• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Watendaji simamieni ununuzi wa dengu na mbaazi Manyara -RC Mkirikiti

Imechapishwa Tarehe: August 13th, 2020

Imeandikwa na: Mariamu Juma, Manyara

Watendaji katika ngazi za Mkoa na Wilaya wametakiwa kushiriana kwa karibu na maafisa ushirika  na viongozi wa vyama vya ushirika kwa ajili ya kusimamia utaratibu wa mazao na ununuzi wa  mazao ya dengu na mbaazi  kwa msimu wa  2020/2021  ili mazao hayo yaweze kukusanywa kupitia  vyama vya ushirika na kuuzwa katika soko la bidhaa  la Tanzania (TMX) ambapo wanunuzi watanunua kwa ushindani kwa utaratibu  utakaowekwa.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti  katika kikao kazi cha wadau wa zao la dengu na mbaazi kilicholenga kupitia na kujadili  rasimu ya mwongozo wa mauzo ya zao la dengu  na mbaazi  kwa msimu wa 2020/2021.

Mkirikiti alieleza kuwa serikali ya awamu ya tano  kupitia wizara ya kilimo  imetoa  maelekezo ya mfumo rasmi ya ununuzi wa zao la ufuta,choroko,dengu,mbaazi na soya  pamoja na waraka wa  Waziri wa kilimo  Na 2 wa mwaka 2020 kuhusu mifumo ya ununuzi wa mazao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani  na vyama vya ushirika.

 Alisema lengo kuu la serikali  ni kusisitiza mfumo huo na kuhakikisha  kuwa kilimo cha mazao husika  kinamnufaisha mkulima hususani mkulima mdogo  sambamba na kuthibiti mfumo holela  wa ununuzi wa mazao hayo ambayo kimsingi  ulikuwa haumnufaishi  mkulima mdogo.

‘’Madhumuni ya kukutana hapa  ni kushikishana katika kupitia mapendekezo ya muongozo wa utaratibu wa mauzo ya mazao   ya dengu na mbaazi  hapa mkoani kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani  kama utekelezaji  wa maagizo ya serikali  ambapo seerikali inataka mfumo huu utumike  katika mauzo ya mazao husika  ili kuhakikisha mkulima anapata soko la uhakika  na lenye manufaa ambapo hii inalenga wadau wote   wanaoshiriki  katika mnyororo wa thamani wa mauzo ya zao husika’’alisema Mkirikiti. 

Hata hivyo Mkirikiti alisema kuwa taarifa alizo nazo ni kuwa Mkoa wa Manyara  tayari umeanza mfumo wa utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi za  ghalani  kwa msimu wa 2019/2020 kwa zao la ufuta kupitia vyama vya ushirika  na soko la bidhaa Tanzania (TMX) ambapo matokeo chanya yamepatikana kwa mkulima kupata bei shindani  ikilinganishwa na uuzaji holela ambapo pia ushuru wa halmashauri uliongezeka , vijana zaidi ya 100 walipata ajira  na mama lishe .

Wakulima walieleza kuwa ili kuendana na mfumo huo ambao serikali imeuweka na walikiri kuukubali ni vyema serikali ikaangalia mfumo  mzuri wa kumuwezesha mkulima anapokuwa na shida  na mazao yake yatakapokuwa tayari akatwe fedha hizo kupitia mazao yake pindi yatakapouzwa.

‘’Tunataka serikali itusaidie  pale tunapokuwa na shida wengine tunasomesha watoto inapotokea nadaiwa ada  ili mwanangu aendelee na masomo  halafu naomba kukopesha kupitia ushirika ili nikivuna mazao yangu muda wa kuuzwa nikatwe hiyo pesa  unakuta haiwezekani  hii inatusukuma sisi kwenda kwa madalali ambao mwisho wa siku wanatunyonya sana sasa kwa kuwa unashida inakubidi uchukue’’Jumanne Shabani ambaye ni  mkulima. 

Aidha Mkuu wa Mkoa huo akatoa wito kuwa mtu yeyote atakayegundulika anaenda vijijini kuwahamasisha wakulima kutokujiunga na mfumo wa stakabadhi ghalani watahakikisha wanamkamata.                         

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.