• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

WAZIRI LUKUVI ATATUA MGOGORO WA SHAMBA LA SINGU MANYARA

Imechapishwa Tarehe: March 7th, 2019

Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi William Lukuvi ametoa majibu ya mgogoro wa Ardhi wa Shamba la Singu lililopo Mkoani Manyara wilayani Babati kata Ya Sigino

Akiwa Katika ziara yake ya kazi Mkoani humo waziri Lukuvi alitoa uamuzi wa mwisho kuhusiana na mgogoro wa shamba hilo uliodumu kwa muda mrefu kati ya mwekezaji na wananchi .

Alisema Wizara yake ilituma wataalamu wake waliokuja kufuatilia historia ya mgogoro huo na hivyo kugundua kuwa shamba hili lilikuwa linamilikiwa na Luten canal  Richard cuper 1926 na baadaye kuuzwa kwa Tanzania Breweries mwaka 1978  Na mwaka 2011  liliuzwa kwa Kampuni ya Agric Evolution Co Ltd  ekari 3113.

Aliongeza kuwa kabla shamba hili kuvamiwa na wananchi kulikuwa na jumla ya hekari 3352 na kaya 11, na Sasa kuna jumla ya kaya 410  zilizogengwa katika shamba hilo  na kufanya shughuli zao za maendeleo  

Kufuatia uvamizi huo Halmashauri ilipanga kubomoa na kuwaondoa wananchi hao waliovamia shamba hilo jambo ambalo Waziri Lukuvi alilipinga na kuwaagiza  kuziacha kaya hizo 410 na kuwazuia wananchi wengine watakaoendelea kuvamia.

"Hatuwezi kuwaondoa na kuwabomolea nyumba zao Wananchi wa kipato cha chini, ardhi ambayo ilishajengwa itaondolewa kwenye umiliki wa Muwekezaji""Serikali tumeamua kutoa ekari 829 kwaajili ya  wananchi waliojenga katika eneo lile ili waweze kujiendeleza na kufanya shughuli za kilimo  na nnaomba mashamba haya muyagawe kwa haki wapewe wahitaji tu,  hatuwezi kuwaacha wananchi wetu bila mashamba" alisema Lukuvi.

 Waziri lukuvi asema shamba hilo ni mali halali ya Kampuni ya Agric Evolution CO Ltd na hivyo kumtaka muwekezaji huyo kukubaliana na maamuzi ya Serikali kwani Uvamizi huo ulisababishwa na wao kutosimamia mali yao ipasavyo.

Lukuvi amezitaka Halmashauri kufuata  sheria na kuwa na desturi ya kumtumia Mwanasheria Mkuu wa Serikali   wanapoingia mikataba ya ardhi na wawekezaji ili kuepusha migogoro isiyo na tija na kusababisha Serikali kushtakiwa.

Aidha aliiagiza Tanesco kuwalipa fidia wananchi ambao mashamba yao yamepitiwa na njia za umeme ambapo asilimia 52 ya fedha hizo zitakwenda kwa wananchi na asilimia 48 kwa mwekezaji.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amewataka wanasiasa kuacha  kuchochea wananchi kuvamia maeneo ya wawekezaji na yale ya Hifadhi kwa matakwa ya kujisafisha na kujitafutia kura kwa wananchi.

"Hii migogoro mingine ilishaisha lakini kuna baadhi ya wanasiasa ndio wanazidi kuichochea,kwa maslahi yao binafsi, msiwatete wananachi wanapotenda maovu kwa kuwa mnataka kura zao" alisema Mnyeti

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.