Mkoa wa Manyara una jumla ya Shule za Msingi 669 (Serikali 620 na binafsi 49) na Shule za Sekondari 172 (Serikali 153 na Binafsi 19) katika Halmashauri saba za Mkoa. Mwaka 2021 Shule za Msingi zina jumla ya wanafunzi 370,121 na sekondari wapatao 63,749.
Shule za Sekondari Kidato cha 5 na cha 6
Mkoa wa Manyara unazo shule 23 za kidato cha 5 na 6, ambazo ni miongoni mwa shule 172 zilizotajwa hapo juu, kwa mchanganuo ufuatao: Babati (W) Shule 2, Babati Mji Shule 4 (moja ya Serikali) Hanang Shule 4, Kiteto Shule 2, Mbulu (W) Shule 2, Mbulu Mji Shule 6 (Tatu za Serikali) na Simanjiro Shule 3. Ili kutekeleza agizo la Serikali la kila Tarafa kuwa na shule moja ya kidato cha 5 & 6 Mkoa na Halmashauri zake unaendelea kuhamasisha ujenzi wa madarasa na mabweni ili kuboresha miundombinu katika baadhi ya Shule za kata ziweze kuwa Shule za Kidato cha 5 & 6. Mwaka huu mwezi Julai, Mkoa
unatarajiwa kusajili shule 4 za kidato cha tano na kufanya jumla ya shule 27
Taasisi za Kielimu katika Mkoa
Katika Mkoa wa Manyara kuna taasisi mbalimbali zinazotoa elimu, taasisi hizi na idadi zake ni kama ilivyo katika mabano; Chuo KiKuu Huria cha Tanzania (1), Vyuo vya Ualimu (2), Vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi - VETA (4), Chuo cha maendeleo ya Wananchi - FDC (1) na Chuo cha Uhasibu (1)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.