Mkoa wa Manyara una Wilaya tano Babati, Kiteto, Mbulu, Simanjiro na Hanang, Mkoa una Halmashauri saba (7) Babati TC, Babati DC, Kiteto, Mbulu DC, Mbulu TC, Simanjiro na Hanang. Utoaji wa huduma ya maji kwa Mkoa wa Manyara umegawanyika katika makundi
matatu;
• RUWASA inashughulikia Vijiji vyote vya Babati DC, Kiteto, Mbulu DC, Sehemu
ya Mbulu TC, Simanjiro, Hanang’ na inasimamia Mamlaka ya Maji Kibaya;28
Tunayo Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Babati (BAWASA) ambayo
pamoja na majukumu yake ya kutoa huduma ya maji kwa Wakazi Babati Mjini
inasimamia utoaji huduma ya maji katika Miji ya Gallapo, Dareda, Magugu na
Bashnet na tarehe 03.08.2021 imekabidhiwa kutoa huduma Katesh baada ya
Mamlaka ile kuvunjwa; na
Mkoa wa Manyara una Mamlaka mbili (2) kwenye Makao MaKuu ya Wilaya
ambazo zinaendelea kuendeshwa chini ya Bodi zao ambazo ni Mamlaka ya Maji Mbulu Mji na Orkesument.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.