JESHI la polisi mkoani Manyara limemkamata mtu mmoja aitwaye Bura Lalay Mayomba mwenye umri wa miaka 55 mkazi wa Kijiji cha Ngoley kata ya Mwada wilaya Babati akiwa na nyara za serikali ambayo ni Mayai ya Mbuni.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Augustino Senga alisema mtuhumiwa huyo Bura Lalay alikamtwa Septemba 03 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi akiwa na Mayai tisa (9) ya Mbuni.
“Afisa wanyama pori katika wilaya ya Babati Jackson Robert, akiwa na askari wa Burunge kwa kushirikiana na askari polisi, wakifanya doria ya muungano, walimkamata mtuhumiwa Bura Lalay Mayomba nyumbani kwake akiwa na mayai tisa ya Mbuni akiwa ameyaficha katika dumu lenye ujazo wa lita 20 nyuma ya nyumba yake.
“Kukamatwa kwa mtuhumiwa na mayai haya tisa ya Mbuni ambayo ni nyara za serikali na kujimilikisha bila kibali au idhini ya serikali/mkurugenzi wa wanyama pori Tanzania.
“Tukio hili limetokana na taarifa za wasamaria wema ambao wana nia njema na rasilimali za serikali. Mtuhumiwa tumemkamata yupo mahabusu na upelelezi ukikamilika tutamfikisha mahakamani," Alisema Senga
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.