Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Alexander Mnyeti leo amekutana na wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani Manyara katika kikao kilichoitishwa katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Mkuu wa Mkoa ili kujadili fursa mbalimbali zipatikanazo katika Mkoa huo.
Akiongea katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wadau wa maendeleo kutoka wilaya zote tano za Mkoa huo Mh.Mnyeti aliwahimiza wadau hao kujitokeza kuanzisha viwanda vipya na kufufua viwanda vilivyokufa hasa katika maeneo ya kilimo,ufugaji,misitu,madini na utalii Mkoani Manyara kwani malioghafi za viwanda zinapatikana kwa urahisi Manyara na pia kutaewaletea ajira wananchi wa Manyara na Tanzania kwa ujumla.
Mh. Mkuu wa Mkoa pia alisisitiza kuwa ifikapo Disemba Mwaka 2018 Mkoa wa Manyara itafikia lengo la kuanzisha viwanda 100 ili kutimiza ahadi ya Rais kuwa kila Mkoa kuwa na viwanda 100 kwani mpaka sasa mkoa umeanzisha viwanda 68 kati ya 100 vinavyohitajika.
Vilevile Mh.Mnyeti alizitaka Halmashauri zote saba zilizopo Mkoanio kwake kuhakikisha zinatenga asilimia tano kwa ajili ya vijana na kinaMama na kuwakopesha bila riba ili kuwawezesha kujikwamua na umaskini.
Akiwasilisha mada katika kikao hicho Mtaalam kutoka TIRDO Dkt.Mushi aliwaambia wadau wa maendeleo kuwa Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa mikioa yenye hali ya hewa nzuri inayokubali kila aina za mazao hivyo kuwahimiza kuwekeza mkoani humo.
Wakichangia mada wadau wa maendeleo mkoani humo wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwaita na kuwaleta wataalam kutoka TIRDO ili kuwafahamisha fursa mbalimbali zipatikanazo mkoani humo.
Mkoa wa Manyara una fursa kama za kilimo cha Mahindi,ufuta,alizeti,mtama,ngano na maharage pia wawekezaji wanaweza kuwekeza kwenye viwanda vya kusindika bidhaa hizo.vilevile kuna fursa za kuanzisha machimbo ya madini, viwanda vya chumvi,viwanda vya Saruji, viwanda vya asali pamoja na viwanda vya mazao ya misitu.
Imeandikwa na: Haji A.Msovu(Afisa Habari Mkoa wa Manyara)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.