Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati n a maji (EWURA) imejipanga kuanzisha mfumo wa vituo vya mafuta vyenye masharti nafuu kwenye maeneo ya vijini ili kukabiliana na biashara ya kuuza mafuta kwenye vifaa visivyoruhusiwa kisheria.
Hayo yamebainishwa na meneja wa EWURA kanda ya kaskazini mhandisi Lorivini Long’idu katika semina kwa wadau mbalimbali Mkoani Manyara na kusema kuwa baadhi ya maeneo hasa ya vijijini yamekuwa yana upungufu ama ukosefu wa vituo vya mafuta hivyo kusababisha adha kwa watumiaji wa vyombo vya moto na katika kutatua changamoto hiyo EWERU imeamua kuja na njia mbadala.
Semina hiyo iliyofunguliwa Novemba 28,2019 na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mh. Elizabeth Kitundu na kuwataka watendaji wa kata,mitaa na vijijini ,maafisa biashara na waandishi wa habari kushirikiana na EWURA ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za umeme,maji na gesi ya kupikia katika Wilaya ya Babati.
“Kutokana na hali hii mamlaka inakuja na mfumo mpya wa vituo vinavyotembea kwa sababu ya uhaba wa mafuta kwa maeneo yasiyo na vituo hivyo hasa ya vijijini na hii itasaidia kupunguza tatizo hili”amesema Long`idu .
EWURA imekuwa na utaratibu wa utoaji wa elimu na semina kwa jamii juu ya mambo mbalimbali ambapo piua imekuwa ikitahadharisha uuzaji na usafirishaji wa mafuta kwa kutumia vyombo vya moto usio rasmi.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.