Wafanyabiashara na wenye vyombo vya moto wametakiwa kuhifadhi Mafuta katika miundombinu sahihi, kama inavyoelekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji, [EWURA] ili kuepuka ajali za moto.
Wito huo umetolewa jana Novemba 28,2019 na Meneja wa EWURA kanda ya Kaskazini Mhandisi Lorivii Long’idu wakati akitoa wasilisho la Mamlaka hiyo kwenye semina maalum ya kuwapa uelewa wa majukumu yao, Watendaji wa kata,Mitaa na Vijiji,Maafisa Biashara na waandishi wa Habari iliyofanyika wilayani Babati mkoani Manyara.
Ewura inasisitiza ujenzi wa vituo vidogo vya Mafuta katika maeneo ya vijijini na kuachana na mbinu za kienyeji za kuhifadhi mafuta kwenye Makopo (Chupa) ili kuepuka ajali zitokanazo na milipuko ya Mafuta ambayo hayajaifadhiwa kitaalamu hali inayopelekea watu kupoteza Maisha na Mali.
Mhandisi Long’idu amesema,EWURA imefanikiwa kutoa leseni 1561 za biashara ya mafuta zikiwemo leseni za biashara ya mafuta ya jumla 66,biashra ya mafuta ya rejareja 1397 na leseni 19 kwa gesi ya kupikia na vilainishi vya mitambo 56
Katika hatua nyingine EWURA ipo kwenye mpango wa kuanzisha Vituo vya mafuta vinavyotembea (Mobile Shell) ili kukabiliana na upungufu wa Mafuta maeneo yasiyokuwa na Vituo vikubwa hususani vijijini.
Mamlaka hiyo imefanikiwa kudhibiti Uchakachuaji wa Mafuta kutoka asilimia 74% kwa mwaka 2007 na hadi kufikia asilima 4% pekee kwa mwaka 2019.
Nao watendaji waliopata elimu hiyo wamesema watakwenda kuitoa kwa wananchi katika maeneo yao ya kazi ili kuwajengea uwezo na kujua njia sahihi ya kutumia huduma zinazosimamiwa na Ewura.
Kwa upande wa maji safi na usafi wa Mazingira Ewura imeshatoa leseni 24 za daraja la tatu za muda wa miaka kumi kwa mamlaka za makao makuu ya mikoa na leseni 81 kwa Mamlaka za maji za miji ya wilaya,Miji midogo na miradi ya maji ya kitaifa.
Aidha imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo gharama kubwa zauendeshaji kutokana na kufanya kazi ya kudhibiti mamlaka 13 za maji,ambapo kati ya hizo 95 ni za wilaya na miji midogo zenye wateja kati ya 4,000 ba 50,000.
Hata hivyo Mamlaka hiyo inashirikiana na wizara ya maji na TAMISEMI katika kuzijengea uwezo wa kuangalia uwezekano wa kuunganisha mamlaka ndogo na kubwa.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.