Bodi mpya ya Hospitali ya rufaa Mkoa wa Manyara imezinduliwa leo tarehe 19/06/2018 katika Jengo la Ofisi za Mkuu wa Mkoa Manyara.
Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhandisi Raymond Mushi aliwataka wajumbe wa Bodi hiyo kushirikiana na wataalam ili kuwaletea huduma bora wananchi wa Mkoa wa Manyara na mikoa ya jirani.
Pia aliwahakikishia wananchi wa Mkoa wa Manyara kuanza kupata huduma zote mara baada ya ujenzi kukamilikam kwani kwa sasa baadhi ya huduma kama X-Ray hazipatikani.
Aidha Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara aliwapongeza wajumbe kwa kuteuliwa kwao kuwa wajumbe wa Bodi hiyo kwani tangu kuanzishwa kwa hospitali hityo haijawahi kuwa na bodi ya ushauri tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha MMgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bwana M.A.R Musa aliwahakikishia wananchi kuwa pamoja na hospitali kuwa chini ya Wizara ya Afya,maendeleo ya jamii,jinsia, wazee na watoto lakini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itahakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kwa kufuatilia maendeleo ya hospitali hiyo.
Akishukuru kwa niaba ya wajumbe wa Bodi hiyo Mwenyekiti wa bodi Dkt.Samwel Ulomi alisema kuwa watajitahidi kadri ya uwezo wao katika kutoa ushauri kwa wataalam wa Hospitali hiyo ili wananchi wafurahie huduma zitolewazo hospitalini hapo.
Wajumbe wa Bodi hiyoni
1.Dkt.Samuel Shilet Ulomi – Mwenyekiti
2.Dkt.Katherine Magali –Katibu
3.Namayani Rapey Edward –Mjumbe
4.Mohamed Arshad Bajwa- Mjumbe
5.Ronald Paul –Mjumbe
6.Dkt.Damas Kayera –Mjumbe
7.Saburi Yakubu –Mjumbe
8.Dkt.Charles Mtabho- Mjumbe
9.Dkt.Yohana Minthey Naasi- Mjumbe
10.Leonard R.Msami –Mjumbe
11.Theonestina Rwechungura-Mjumbe
12.Abdallah Kilobwa-Mjumbe
Imeandikwa na: Haji A.Msovu(Afisa Habari Mkoa wa Manyara)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.