Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameonyesha matumizi bora ya utekelezaji wa miradi bila kutumia mkandarasi maarufu kama ‘Force Account ‘ kwa Makatibu Tawala wa Mikoa ,Wenye viti wa Halmashauri, Wakurungezi na Maafisa mipango wa Halmashauri kwa kuwapeleka kwenye mradi wa Ofisi za Jengo la Ofisi ya Rais TAMISEMI linaloendelea kujengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Jafo amefanya ziara hiyo baada ya kikao chake cha maelekezo kwa viongozi hao ambao halmashauri zao zilifaulu vigezo na kusaini fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati awamu ya Pili.
Akizungumzia Force Account Jafo alisema kuwa nimeamua kutekeleza kwa vitendo yale ninayowaagiza wakati wote wa maelekezo yangu kuhusu kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yenu.
Katika ujenzi wa Jengo hili la Ofisi za Wizara tuliamua na kukubaliana kwa pamoja kutumia mfumo ule ule ambao unatumika katika halmashauri zetu sio sisi tunatoa tu maagizo lakini hatutendi na sasa kupitia mradi huu tumeamua kuwa mfano halisi wa yale tunayoyazungumza alisema Jafo.
Aliongeza kuwa katika mfumo huu wa force Account tumeweza kusimamia jengo hili kupitia kamati nne ambazo ni Kamati ya manunuzi, Kamati ya Vifaa, Kamati ya ujenzi na ile ya usimamizi na ufuatiliaji.
“Mradi huu umekuwa na tija pia kwa jamii kwani umetengeneza ajira kwa vijana wetu kwani wao ndo wamekua nguvu katika kufanya shughuli zote za ujenzi kuendelea kwa mujibu wa maelekezo ya wahandisi ambao wanatokea Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na msimamizi wa mradi huu”Amesema Jafo
Wakati huo huo Jafo aliongeza kuwa ujenzi wa Jengo hili la kisasa zaidi linagharimu shilingi billion moja tu Fedha zilizo tolewa na Rais Magufuli kwa kila Wizara kwa ajili ya kujenga Ofisi katika Mji wa Serikali Ihumwa.
“Nataka niwahakikishie kuwa ujenzi wa jengo hilo umeratibiwa na mimi mwenyewe Waziri wa TAMISEMI ambapo niliwaunganisha viongozi wote wakuu wa Wizara pamoja na watendaji wa Wizara ili kuleta matokeo makubwa na ya haraka”
Sasa kama mimi nimeweza wewe kwanini ushindwe na jengo hili limeanza kujengwa mwezi Disemba 2018 na kama mnavyoona sasa hivi jengo limeshafikia hatua ya mtamba wa panya kwahiyo kasi ya ujenzi iko vizuri sana na tutamaliza ujenzi huu ndani ya muda mfupi ujao; Nataka na nyie mkafanye hivi kwenye maeneo yenu alimalizia Jafo.
Kwa kuongezea Jafo amazitaka halmashauri zilizo pata fedha ya kutekeleza miradi ya Kimkakati kuanza mipango ya utekelezaji wa miradi hiyo mapema iwezekanavyo ili fedha hizo zitakapowasili katika halmashauri hizo miradi ianze mara moja na ili iweze kumalizika kwa wakati uliopangwa.
Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Eng. Zenah Saidi ametoa shukrani za dhati kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa fedha hizo na kuhaidi kusimamia kwa umakini na kuhakikisha zinatekeleza miradi husika kwa ufasaha na ubora wa miradi hiyo kuendana na thamani ya fedha hiyo.
“Nitoe wito kwa viongozi wa halmashauri kuwa sasa ni wakati wa kutekeleza miradi hii kwa kutumia mfumo wa Force Account kwani kila mmoja wetu kapata kushuhudia kwa macho yake namna ya mfumo huu unavyo tumika na faida zake kazieleza Bi.Zenah
Kwa kuhitimisha Bi.Zena amewataka viongozi wenzake kuwa makini wakati wa kutafuta wakandarasi wa kutekeleza miradi kwa wengi wao katika makaratasi wanakuwa vizuri lakini katika utekelezaji hakuna kitu.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.