Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh.Selemani Jafo amezitaka Kamati za Rufaa za Uchaguzi wa Serikali za kutenda haki kwa wagombea wote watakaowasilisha malalamiko yako kuhusu uteuzi.
Waziri Jafo aliyasema hayo siku ya Jumatano ya tarehe 6/11/2019 wakati akizungumza na Kamati za Rufaa pamoja na viongozi wa Mkoa wa Manyara katika ziara yake Mkoani humo kuangalia maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Amesema tunataka haya malalamiko yanayoendelea huko nje hivi sasa yaishe na kuisha kwake ni nyinyi wajumbe wa Kamati hizi kufanya kazi zenu kwa umakini na uadilifu mkubwa ili kuhakikisha haki inatendeka. ” Tunategemea sana Kamati hizi za Rufaa zilizoundwa katika kila Wilaya Nchini kote katika kutenda haki na kuweka mambo yote sawa ili kila mtu awe na amani na tukamilishe zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa salama” Alisema Jafo.
Aliongeza kuwa katika mchakato huu msimuonee aibu yoyote na wala msimpendelee mtu, katendeni haki kwa watu watakaoleta malalamiko yao kwenu ili kila mtu afurahie uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ukamilike kwa amani.
Ndio maana mmechaguliwa kutoka Taasisi za Umma mbalimbali na hamkutoka katika ofisi moja kila mmoja wenu katoka kwenye Taasisi yake,hii itasaidia kupunguza mgongano wa maslahi kwa kuwa nyinyi hamfanyi kazi katika Serikali za Mitaa. “Pimeni malalamiko kwa weledi wenu na kufuata kanuni, toeni maamuzi stahiki,inawezekana kabisa kamati ya Rufaa ikamrudisha mtu kwenye nafasi yake ambayo alieguliwa hapo awali mkiona anastahili kwa mujibu wa vielelezo alivyowasilisha mrejesheni,hiyo ndio kazi yenu kubwa katika kamati hizi” Alisistiza Jafo.
Waziri Jafo aliongeza kwa wanaogombea wote amabao wanaona kuna baadhi ya vitu havikwenda sawa huu ndio wakati sasa wa kuwasilisha vielelezo vyao kwa Kamati ya Rufaa ili viweze kuhakikiwa na kufanyiwa maamuzi ya busara yanayofuata utaratibu,sheria na maelekezo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni uchaguzi wa wananchi, ni vyema michakato yote ikafanyika kwa haki kwenye ngazi zote haswa hii ya kugombea nafasi za uongozi haki inatakiwa kuonekana imetendeka hivyo Kamati za Rufaa nawaelekeza fanyani kazi.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.