Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji *CGF* . John W. Masunga jana tarehe 27.O2.2O2O amefanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Manyara kwa ajili ya kukagua utendaji kazi wa Jeshi hilo, alifika Manyara akitokea Mkoani Arusha ambapo ni ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Akiwa mkoani Manyara Kamishna Jenerali amewaasa Maafisa na Askari kuongeza bidii kwenye kazi za uzimaji Moto na Uokoaji pamoja na kuzingatia Nidhamu kwenye utekelezaji wa Majukumu Jeshi.
Kamishna Jenerali alihimiza zaidi juu ya utoaji wa elimu kwa Umma ili kuzuia na kupunguza Majanga ya Moto kutokea, ukizingatia siku za hivi karibuni kumekuwa na uunguaji wa Masoko na kusababisha madhara kwa jamii.
Ufunguaji wa Vilabu wa marafiki wa Zimamoto Shuleni ni eneo alilogusia, na kusisitiza vilabu zaidi vianzishwe na viwe hai na vilivyopo viimarishwe.
Aidha aliwasisitiza Maafisa na Askari kujiepusha na vitendo vya Rushwa.
Kamishna Jenerali alihitimisha, kwa kuwaeleza Maafisa na Askari juu ya changamoto zilizopo za vitendea kazi na kueleza anazifahamu na serikali inafanyia kazi.
Awali kabla ya Kuongea na Maafisa na Askari alifika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kusalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexander Mnyeti.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.